41. Msimamo juu ya magomvi yaliyotokea kati ya Maswahabah

Wanaona kwamba mtu anapaswa kukomeka na yale magomvi yaliyotokea kati ya Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mtu asiwazungumze kwa njia ya kuwatia kasoro au mapungufu. Wanaona kwamba mtu anapaswa kuwatakia rehema wote na kuwapenda wote. Vilevile wanaona kwamba inatakiwa kuwatukuza wakeze (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwaombea du´aa. Aidha inatakiwa kutambua fadhilah zao na kukubali ya kwamba wao ni mama wa waumini.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 294
  • Imechapishwa: 25/12/2023