41. Inafaa kuwapiga vita wezi na Khawaarij

Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

“Inafaa kuwapiga vita wezi na Khawaarij. Wakimshambulia mtu au mali yake basi inafaa kwake kupambana kwa ajili ya nafsi yake na mali yake. Ajitetee kwa yote ayawezayo. Hata hivyo haifai kwake kuwafuata au kuwatafuta wakimuacha. Hakuna mwingine isipokuwa kiongozi au mtawala wa waislamu ndiye anayeweza kufanya kitu kama hicho. Ana haki tu ya kujitetea mahala hapo. Anuie kutomuua yeyote. Ikitokea wakati wa kuitetea nafsi yake akamuua yule mshambulizi, basi atajaza yule mshambulizi.”

MAELEZO

Kuwapiga vita waasi, wezi na Khawaarij inafaa pindi watapomvamia mtu au mali yake. Wakitaka kuvunja heshima ya familia ya mtu basi ni lazima kwake kuitetea. Inafaa kwake kuitetea nafsi yake na mali yake na ni lazima kuitetea familia yake kwa njia zote anazoweza.

Katika kipande hichi Imaam Ahmad ametilia mkazo kwamba mtu asifuatilie nyayo zao wakimwacha salama yule mshambuliwaji na wakakimbia. Kwa sababu ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) wakati alipopigana na Khawaarij aliamrisha wasifuatiliwe iwapo watakimbia[1]. ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) ni mmoja katika wale makhaliyfah waongofu ambaye mwenendo wake unatakiwa kufuatwa.

[1] al-Bayhaqiy katika ”as-Sunan al-Kubraa” (16521).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Itmaam-ul-Minnah, uk. 147-148
  • Imechapishwa: 01/05/2019