40. Neno na kucheka kwa Allaah ni tofauti na viumbe

Vivyo hivyo kuhusu neno la Allaah. Allaah anasema, lakini sio kama wanavosema viumbe. Wito Wake sio kama wivo wa viumbe. Maneno ya Allaah sio kama maneno ya viumbe. Sifa za Allaah ni zenye kulingana Naye na Yeye ndiye Mwenye kumuitikia mwombaji:

“Ni nani mwenye kuniomba nimjibie? Ni nani mwenye kuniuliza nimpe? Ni nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe?”

Hakika Yeye ni Mwingi wa kutoa na ni Mkarimu (Subhaanahu wa Ta´ala). Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. Ni wajibu kumthibitishia Allaah sifa hizi kwa njia inayolingana Naye. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah anawacheka watu wawili ambapo mmoja wao kamuua mwenzake. Halafu wote wawili wanaingia Peponi.”

Ni kucheka kunakolingana na Allaah. Hashabihiani na viumbe Vyake katika sifa zao na kucheka kwao. Bali sifa za Allaah zinalingana Naye na zinahusiana Naye (Jalla wa ´Alaa). Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tena:

“Anastaajabu Mola Wetu kwa kukata tamaa waja Wake licha ya mabadiliko Yake ya hali zao yako karibu. Huwatazama mnapokuwa katika hali ngumu na wenye kukata tamaa. Huanza kucheka kwa kuwa Anajua kuwa faraja yenu iko karibu.”

Bi maana mambo yako karibu kubadilika. Mtu wakati mwingine anaweza kukata tamaa kutokana na hali ngumu licha ya kwamba faraja ya Allaah iko karibu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 57-58
  • Imechapishwa: 23/10/2024