72. Hadiyth tele juu ya kushuka kwa ad-Dajjaal na ´Iysaa

Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

123 – Tunaamini alama za Qiyaamah, kukiwemo kujitokeza kwa ad-Dajjaal na kushuka kwa ´Iysaa mwana wa Maryam (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokea mbinguni.

124 – Tunaamini kuchomoza kwa jua upande wa magharibi na kujitokeza kwa Mnyama ardhini kutoka maeneo pake.

MAELEZO

Hadiyth juu ya hayo zimepokelewa kwa wingi sana (متواتر), kama walivyoshuhudia hilo wengi katika maimamu mabingwa. Nina kitabu juu ya mada hiyo kwa jina ”Qisswat-ul-Masiyh ad-Dajjaal wa Nuwzuli ´Iysaa (´alayhis-Salaam) wa Qatlihi Iyyaah”. Namuomba Allaah aniwepesishie kukisafisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 107-108
  • Imechapishwa: 20/10/2024