Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Msingi wa tatu ni kumtambua Mtume wenu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alikuwa ni Muhammad bin ´Abdillaah bin ´Abdil-Muttwalib bin Haashim. Haashim alikuwa anatokamana na [kabila la] Quraysh, Quraysh ni kutokamana na waarabu na waarabu ni kutokamana na kizazi cha Ismaa´iyl, mtoto wa Ibraahiym al-Khaliyl – baraka za juu na salaam ziwe juu yake na kwa Mtume wetu.

MAELEZO

Huu ndio msingi wa tatu; kumtambua Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni lazima kwa mtu kumjua Mtume wake ambaye Allaah kamtumia, akafikisha ujumbe, akambainishia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Shari´ah ambazo Allaah amemuamrisha na akamuwekea wazi ´ibaadah ambazo Allaah ametuumba kwa ajili yake.

Mtume huyu ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yeye ndiye Mtume wa mwisho na ndiye Mtume wa Allaah kwa watu na majini wote. Allaah amemtuma kwa watu wote. Amesema (Ta´ala):

قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا

“Sema: “Hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu nyinyi nyote.”” (07:158)

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِّلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

“Hatukukutuma isipokuwa kwa watu wote uwe mbashiriaji na muonyaji, lakini watu wengi hawajui.” (34:28)

Anaitwa Muhammad, Ahmad, al-Haashir, al-Maahiy na Muqaffaa kwa kuwa yeye ndiye Mtume wa mwisho. Yeye ni Mtume wa tawbah, Mtume wa huruma na Mtume wa kichinjwa. Yote haya ni majina yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini ambalo linajulikana, bora na tukufu zaidi ni Muhammad alilopewa na familia yake na ndilo lililotajwa katika Qur-aan. Amesema (Ta´ala):

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ

“Muhammad ni Mtume wa Allaah.” (48:29)

Vivyo hivyo Ahmad. Jina hili ndilo alilokuwa akitumia ´Iysaa pindi anapotoa bishara njema juu yake:

وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِن بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ

“Pindi ‘Iysaa, mwana wa Maryam, aliposema: “Enyi wana wa Israaiyl! Hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat na mwenye kubashiria kuja kwa Mtume baada yangu jina lake ni Ahmad.” (61:06)

Anaitwa Muhammad, baba yake anaitwa ´Abdullaah, babu yake anaitwa Shaybah, lakini alikuwa akiitwa ´Abdul-Muttwalib, na baba wa babu yake alikuwa anaitwa Haashim.

Haashim alikuwa mkubwa katika wakubwa wa Quraysh, kadhalika ´Abdul-Muttwalib. Haashim alikuwa anatokamana na Quraysh ambayo ndio kabila kubwa na waarabu bora kabisa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa ndiye mbora wa kabila hilo na kutokamana na kizazi cha Haashim. Haashim ndio kizazi bora cha Quraysh. Imesemekana kuwa Quraysh alikuwa ni mwanaume kwa jina Fihr bin Maalik. Imesemekana vilevile kuwa alikuwa akiitwa an-Nadhwr bin Kinaanah, babu yake na Fihr bin Maalik. Quraysh ni katika wale waliokuwa waarabu na wakajifunza lugha ya kiarabu. Wakapata lugha ya kiarabu ya wazi. Ni waarabu wengi kuliko Qahtwaan. Kwa ajili jii huwa ikisemwa kuwa kuna waarabu wenye msingi wa kiarabu na kuna waarabu waliokuwa waarabu ambao ni katika kizazi cha Ismaa´iyl, ambaye ni mwana wa Ibraahiym kipenzi wa karibu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 47-48
  • Imechapishwa: 02/02/2017