40. Haifai kufanya mapambano na uasi dhidi ya mahakama

Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

“Si halali kumpiga vita mtawala. Asiwepo mtu yeyote atakayemfanyia uasi. Atakayefanya hivo basi ni mtu wa Bid´ah aliye mbali na Sunnah na njia iliyonyooka.”

MAELEZO

Allaah (´Azza wa Jall) ameamrisha kumtii kiongozi midhali ni muislamu. Haijuzu kumfanyia uasi ijapokuwa atadhulumu, atakupiga mgongo wako na kuchukua mali yako. Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msikilizeni na mumtii kiongozi hata kama atakupiga mgongo wako na kuchukua mali yako. Msikilizeni na mumtii!”[1]

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaona kuwa haijuzu kufanya uasi dhidi ya kiongozi midhali hajaingia katika ukafiri wa wazi kabisa ambao kuna dalili kutoka kwa Allaah. Ahl-ul-Bid´ah tu kama Khawaarij na Mu´tazilah ndio wenye kujuzisha kufanya uasi dhidi ya kiongozi.

Hivyo basi kuwa pamoja na wale wenye kufuata na jiepushe mbali na wale wenye kuzusha. Njia yao ndio njia iliyonyooka na inahusiana na kushikamana barabara na mapokezi.

[1] Muslim (1847).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Itmaam-ul-Minnah, uk. 145-146
  • Imechapishwa: 01/05/2019