10- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mmoja wenu kutoka asubuhi na kuokota kuni na kubeba mgongoni, akatoa swadaqah kwa kuni hizo na akajitosheleza na watu ni bora kwake kuliko kumuomba mtu ambaye ima atampa au kumnyima. Hilo ni kwa sababu mkono ulio juu ni bora kuliko mkono ulio chini. Anza na yule aliye chini yako.”[1]

Mlango huu na ulio kabla yake unarejea katika maana moja nayo ni kwamba haijuzu kuwaomba viumbe isipokuwa wakati wa dharurah tu. Hali kama hiyo ni pale ambapo mtu atakutana na umasikini mkubwa. Mbaya kuliko hiyo ni pale ambapo mtu atakuwa hana mali yoyote kabisa.

11- ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhu) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Sio halali kumpa swadaqah tajiri wala aliye na nguvu.”[2]

ash-Shaafi´iy, Abu Thawr na wengine wanafuata Hadiyth hii katika mlango huu na kusema ya kwamba haijuzu kumpa swadaqah kila ambaye ana nguvu za kutosha za kuchuma riziki yake, kupata kazi na kusimamia pesa vizuri ili asihitajie kuwaomba watu. Vilevile linawahusu Suufiyyah ambao wameacha kufanya kazi na kujishughulisha na kufanya ´ibaadah. Sio halali kuwapa swadaqah. Kuacha ´ibaadah za Sunnah kwa ajili ya kutafuta riziki ni jambo linalokuja mbele ya riziki iliyoachwa kwa kuwaomba watu.

12- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kitu bora anachokula mtu ni kile chenye kutokamana na kazi ya mikono yake.”

[1] Muslim (1042) na at-Tirmidhiy (680)

[2] Ahmad (6530), Abu Daawuud (1617), at-Tirmidhiy (647) na ad-Daarimiy (1646).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad al-Qurtwubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Hirsw biz-Zuhd wal-Qanaa´ah, uk. 18-20
  • Imechapishwa: 18/03/2017