39. Mwenye tumbo kubwa na tumbo lake

222 – Muhammad amesema: Yahyaa bin Ishaaq ametuhadithia: an-Nadhwr bin Ismaa´iyl ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Abiyr-Rabbaab: ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz amesema:

”Aangamie yule ambaye tumbo ndio hamu yake kubwa.”

223 – Muhammad amesema: Mu´aadh Abu´Awn ametuhadithia: Nimemsikia Buhaym Abu Bakr al-Kuufiy al-´Aabid akisema:

”Tumefikiwa na khabari kwamba wenye njaa kwa ajili ya Allaah watakusanywa maeneo palipoinuka siku ya Qiyaamah, kisha wawekewe meza ya chakula na kuambiwa: ”Kuleni kwa raha zenu. Kunyweni kwa raha zenu kutokana na ile njaa mliyopata kwa ajili ya Allaah duniani.” Watakula na kunywa wakati ambao watu watakuwa wanafanyiwa hesabu.”

224 – Muhammad amesimulia: Zakariyyaa bin ´Adiy ametuhadithia: Ja´far bin Sulaymaan ametuhadithia: Nimemsikia Farqad as-Sabkhiy akisema:

”Ole wake mwenye tumbo kubwa kutokana tumbo lake! Akihisi njaa, analinyongesha, na akishiba, analipa uzito.”

225 – Muhammad bin Salaam al-Jamhiy ametuhadithia: ´Umar bin Abiy Khaliyfah ametuhadithia:

Bwana mmoja alisema kumwambia al-Hasan: ”Ee Abu Sa´iyd! Nikila kidogo, nanyongeka, na nikila sana, nabweteka.” Akasema: ”Tafuta nyumba nyingine.”

226 – Muhammad amesema: ´Ubaydullaah bin Muhammad at-Taymiy amenihadithia: ´Uqaybah bin Fadhwaalah amenihadithia, kutoka kwa mmoja katika marafiki zake, ambaye amesema:

”Nimesoma kwenye kitabu kimoja: ”Allaah hajataamiliana na watu kwa kitu kilicho bora kama kuwa na njaa kwa kipindi kirefu.”

227 – Muhammad amesema: Suurah bin Qudaamah al-Aswaariy ametuhadithia: Hayyaan bin al-Aswad ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdul-Khaaliq bin Muusa al-Laqiytwiy, ambaye amesema:

”Yaziyd ar-Raqaashiy aliifanya nafsi yake kuwa na njaa kwa ajili ya Allaah miaka sitini, mpaka mwili wake ukakauka na kuchoka na rangi ya mwili wake ikabadilika. Alikuwa anasema: ”Tumbo lake limenishinda. Sina njia nyingine.”

228 – Muhammad bin Idriys amenihadithia: ´Abdah bin Sulaymaan ametuhadithia, kutoka kwa Ibn-ul-Mubaarak, kutoka kwa Ja´far bin Sulaymaan, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Marwaan al-Muhallimiy, ambaye amesema:

”Nilisema kumwambia Maalik bin Diynaar: ”Nimefikiwa na khabari kwamba matunda yanakuja na kuondoka bila ya kuonja chochote.” Akasema: ”Majivu yangenitosha, basi nisingekula kitu kingine mpaka nijue ni nini atachonifanya Mola wangu.”

229 – Muhammad bin Idriys amenihadithia: Sunayd bin Daawuud ametuhadithia: Ja´far bin Sulaymaan ametuhadithia:

”Wakati Maalik bin Diynaar alipotaka kukata roho, alisema: ”Ee Allaah! Nataraji ujue kutoka moyoni mwangu kwamba mimi sijui sipendi maisha na nayachukia mauti kwa sababu ya tumbo langu na si kwa ajili ya tupu yangu.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 139-142
  • Imechapishwa: 31/07/2023