Swali: Inasihi kufunga siku tatu kila mwezi kwa kuachanisha?

Jibu: Ni mamoja muislamu amefunga mwanzoni mwa mwezi, katikati yake au mwishoni mwake, swawm yake inasihi. Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Ameniusia mwandani wangu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mambo matatu: kufunga siku tatu kila mwezi, swalah ya Dhuhaa na kuswali Witr kabla sijalala.”[1]

Lakini katika Hadiyth ya Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh) masiku yamebainishwa kwamba ni tarehe kumi na tatu, tarehe kumi na nne na tarehe kumi na tano za kila mwezi. Yule mwenye kudhibiti masiku haya Meupe, amefanya vizuri, na yule mwenye kuyaachanisha hakuna neno juu yake.

[1] al-Bukhaariy (1178), Muslim (721), at-Tirmidhiy (760), an-Nasaa’iy (1677), Abu Daawuud (1433) na Ahmad (7098, 7140 na 7409).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 35
  • Imechapishwa: 01/04/2022