38. Amekunywa juisi bila kujua kama alfajiri imekwishaingia

Swali: Miaka kadhaa iliyopita niliamka kutoka usingizini katika Ramadhaan na sikuwa na uhakika kama kumeshaadhiniwa kwa ajili ya Fajr au bado. Nikanywa juisi na tahamaki nikasikia kunakimiwa swalah. Nifanye nini?

Jibu: Ni lazima kwako kuilipa siku hiyo na hakuna kinachokulazimu zaidi ya hivo. Ni lazima kwako kuhakikisha wakati mwingine.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 35
  • Imechapishwa: 01/04/2022