Muslim amepokea katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa Abu Hassan aliyesema:

“Watoto wangu wawili wa kiume walifariki. Nikamuuliza Abu Hurayrah kama anaweza kuwa amesikia kitu kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambacho kinaweza kuwafanya wakawa na furaha baada ya wafiliwa wetu. Akasema: “Ndio. Watoto wao ni vijana wa Peponi. Watakutana na baba zao – au wazazi wao – na wawashike nguo zao – au mikono yao – kama ninavyokushika nguo zako na hawatowaacha mpaka pale Allaah atapowaingiza Peponi wao na baba zao.”

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kuwaambia wanawake:

“Hakuna mwanamke yeyote kati yenu atayefiwa na watoto watatu isipokuwa watakuwa ni ngao kwake kutokamana na Moto.” Mwanamke mmoja akasema: “Watoto wawili?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Na wawili.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 72-74
  • Imechapishwa: 14/10/2016