38. Liwazo la Mtume kwa wazazi waliofiliwa na wanao

Hadiyth hizi zilizo na matamshi mbalimbali, lakini zilizo na maana moja, zinaonyesha kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alizitamka katika minasaba mbalimbali. Zinaonyesha dalili vilevile jinsi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anavyoujali Ummah wake na kuuhurumia. Hadiyth zote zinauliwaza Ummah juu ya wale watoto wanaofiliwa. Zinaonyesha kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametaka kuwaliwaza wazazi waliofiliwa na watoto wao kwa kuwaeleza zile thawabu kubwa zinazowasubiri kwa ajili ya misiba na wasubiri kwa ajili ya hilo. Wazazi wakiongezea juu ya hilo kuridhia msiba ule, kuwaficha watu na kuupokea, ni fadhila za Allaah anazompa yule Amtakaye – na Allaah ni Mwingi wa fadhila.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 70-71
  • Imechapishwa: 14/10/2016