25 – Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba alimwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Nifunze du´aa nitayoomba ndani ya swalah yangu.” Akamwambia: “Sema:

اللّهُـمَّ إِنِّـي ظَلَـمْتُ نَفْسـي ظُلْمـاً كَثـيراً وَلا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْت، فَاغْـفِر لي مَغْـفِرَةً مِنْ عِنْـدِك وَارْحَمْـني إِنَّكَ أَنْتَ الغَـفورُ الرَّحـيم

”Ee Allaah! Hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu dhuluma nyingi na hakuna asamehaye dhambi isipokuwa Wewe. Hivyo basi, nisamehe msamaha kutoka Kwako na unirehemu. Kwani hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Kwa Muslim imekuja namna hii:

كَبِيرًا ظُلْمًا

“Dhuluma kubwa.”[2]

[1] al-Bukhaariy (6326) na Muslim (2705).

[2] Maana yake imekwishatangulia katika Hadiyth ya (25).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 113
  • Imechapishwa: 05/11/2025