116 – ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Miongoni mwa mambo ya mwisho anayosema baina ya Tashahhud na Tasliym ilikuwa ni:

اللّهُـمَّ اغْـفِرْ لي ما قَدَّمْـتُ وَما أَخَّرْت، وَما أَسْـرَرْتُ وَما أَعْلَـنْت، وَما أَسْـرَفْت، وَما أَنْتَ أَعْـلَمُ بِهِ مِنِّي أَنْتَ المُقَـدِّمُ، وَأَنْتَ المُـؤَخِّـرُ لا إِلهَ إِلاّ أَنْـت

“Ee Allaah! Nisamehe niliyoyatanguliza, niliyoyachelewesha, niliyoyafanya kwa siri, niliyoyafanya kwa dhahiri, niliyochupa mpaka na ambayo Wewe unayajua zaidi kuliko mimi. Wewe ni mwenye kutanguliza na Wewe ni mwenye kuchelewesha – hapana mungu wa haki mwengine isipokuwa Wewe.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Du´aa hii, ni kama tulivyotangulia kutaja[2], kwamba imethibiti katika “as-Swahiyh” ya Muslim kuwa inasemwa baada ya Tashahhud kabla ya salamu na baada ya salamu.

[1] Muslim (771).

[2] Maana yake imekwishatangulia katika Hadiyth (28).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 113
  • Imechapishwa: 05/11/2025