113 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Anapokaa Tashahhud mmoja wenu basi amwombe kinga kwa Allaah kutokamana na mambo manne:
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ جَهَنَّمَ، وَمِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ، وَمِنْ فِتْنَةِ الْمَحْيَا وَالْمَمَاتِ، وَمِنْ شَرِّ فِتْنَةِ الْمَسِيحِ الدَّجَّالِ
“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba ulinzi kutokamana na adhabu ya Moto, kutokamana na adhabu ya kaburi, kutokamana na fitina ya uhai na kifo na kutokamana na fitina ya al-Masiyh ad-Dajjaal.”
Imekuja katika tamko la Muslim:
“Atakapomaliza mmoja wenu Tashahhud ya mwisho.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
114 – ´Aaishah, mkewe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), amesimulia kwamba alikuwa akiomba ndani ya swalah:
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ الْمَسِيحِ الدَّجَّالِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ الْمَحْيَا وَالْمَمَاتِ اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْمَأْثَمِ وَالْمَغْرَمِ
“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba ulinzi kutokamana na adhabu ya kaburi. Nakuomba ulinzi kutokamana na fitina ya al-Masiyh ad-Dajjaal. Nakuomba ulinzi kutokamana na fitina ya uhai na kifo. Ee Allaah! Nakuomba ulinzi kutokamana kutokamana na madhambi na madeni.”[2]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
115 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitufunza du´aa hii kama anavyotufunza Suurah katika Qur-aan. Akisema: “Semeni:
اللَّهُمَّ إِنَّا نَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ جَهَنَّمَ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ الْمَسِيحِ الدَّجَّالِ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ الْمَحْيَا وَالْمَمَاتِ
“Ee Allaah! Hakika sisi tunakuomba ulinzi kutokamana na adhabu ya Moto. Nakuomba ulinzi kutokamana na adhabu ya kaburi. Nakuomba ulinzi kutokamana na fitina ya al-Masiyh ad-Dajjaal. Nakuomba ulinzi kutokamana na fitina ya uhai na kifo.”[3]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Katika Hadiyth hii kuna uwekwaji wa Shari´ah wa kumuomba ulinzi Allaah kutokamana na mambo haya manne katika Tashahhud ya mwisho baada ya kumaliza kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kabla ya Tasliym kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi. Kuhusu Tashahhud ya kwanza hakuna du´aa baada ya Tashahhud hiyo.
Makusudio ya ´fitina ya uhai` ni yale yanayomkumba mtu katika maisha yake katika kushughulishwa na dunia, matamanio, hoja tata na vita. Khatari zaidi ni mwisho mbaya.
Na ´fitina ya kifo` ni ile fitina wakati wa kufa. Inafaa pia ikawa imekusudiwa fitina ya ndani ya kaburi, ambao ni mtihani mkubwa, kama ilivyotajwa katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy:
“Nimeteremshiwa wahy ya kwamba mtapewa mtihani ndani ya makaburi kama – au karibu na – mtihani wa al-Masiyh ad-Dajjaal.”
ad-Dajjaal ni bwana ambaye atajitokeza katika zama za mwisho ambaye ataanza akiwa ni mwenye kudai kuwa ni mwema, kisha adai kuwa ni Nabii na hatimaye adai kuwa yeye ndiye mola. Miongoni mwa mtihani wake mkubwa ni kuwa yule ambaye atamtii maisha yake yatakuwa ya starehe na ambaye atamuasi maisha yake yatakuwa yenye dhiki.
Madhambi yake maana yake ni yale yanayopelekea kunako madhambi.
Madeni ni yale madeni anayokuwa nayo mtu na kudaiwa nayo.
[1] al-Bukhaariy (832) na Muslim (589).
[2] al-Bukhaariy (1377) na Muslim (588).
[3] Muslim (590).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 111-112
- Imechapishwa: 05/11/2025

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 111-112
Imechapishwa: 05/11/2025
https://firqatunnajia.com/37-duaa-baada-ya-tashahhud-kabla-ya-tasliym/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket