118 – Sa´d bin Abiy Waqqaas (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akiamrisha mambo haya matano na akiyasimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

اللَّهمَّ إنِّي أعوذُ بِكَ منَ البُخلِ ، وأعوذُ بِكَ منَ الجُبنِ وأعوذُ بِكَ أن أَرَدَّ إلى أرذلِ العمرِ ، وأعوذُ بِكَ مِن فتنةِ الدُّنيا ، وأعوذُ بِكَ مِن عذابِ القبرِ

“Ee Allaah! Hakika mimi najilinda Kwako kutokana na ubakhili, najilinda Kwako kutokana na woga, najilinda Kwako kutokana na kurudi katika umri dhalili, najilinda Kwako kutokana na mtihani wa dunia, najilinda Kwako kutokana na adhabu ya kaburi.”

Imekuja katika tamko jengine:

“Sa´d alikuwa akiwafunza watoto wake maneno haya kama ambavo mwalimu anawafunza wanafunzi wake na akisema:

“Hakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akijikinga nayo baada ya kila swalah.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy.

MAELEZO

Neno (دبر الشيء) makusudio ni mwishoni mwake. Neno (دبر الصلاة) ni mwishoni mwake katika Tashahhud. Alikuwa akisema hivo mwishoni mwa Tashahhud. Mswaliji anatakiwa kuomba du´aa hizi. Aidha imamu anatakiwa kuwawezesha jambo hilo waswaliji mwishoni mwa Tashahhud.

[1] al-Bukhaariy (6370).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 114
  • Imechapishwa: 05/11/2025