38. Mfano wa Radd ya kijumla juu ya utata wa washirikina

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Katika yale niliyokutajia, ni pamoja na kwamba Allaah kataja kuwa washirikina walikuwa wanakubali matendo MYake na kwamba kukufuru kwao ilikuwa ni kwa kujikurubisha kwao kwa Malaika, Mitume, mawalii kwa kusema kwao:

هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ

“Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.” (10:18)

Hili ni jambo la lililo wazi na wala hawezi yeyote kubadilisha maana yake.

MAELEZO

Mtunzi (Rahimahu Allaah) anabainisha jinsi tutavyorudisha Aayah zenye kutatiza katika Aayah zilizo wazi. Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kuwa washirikina walikuwa wakithibitisha na wakiamini Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Hata hivyo walikuwa wakiwaabudu malaika na wengine na wakisema kuwa ni waombezi wao mbele ya Allaah. Pamoja na hivyo walikuwa washirikina ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alihalalisha damu na mali zao. Hili ni andiko lililo wazi na wala hawezi yeyote kubadilisha maana yake. Linafahamisha ya kwamba Allaah hana mshirika katika ´ibaadah Yake, vivyo hivyo hana mshirika katika uola na ufalme Wake. Hii ni shirki, hata kama mtu atathibitisha kuwa Allaah amepwekeka katika uola Wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 57-58
  • Imechapishwa: 11/11/2023