39. Hakuna mgongano katika maneno ya Allaah na Mtume Wake

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Wewe mshirikina! Sielewi maana ya uliyoyataja katika Qur-aan au maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), lakini nina uhakika ya kwamba maneno ya Allaah hayagongani, na kwamba maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hayaendi kinyume na maneno ya Allaah.

MAELEZO

Maneno yake “Sielewi maana ya uliyoyataja… ” anamaanisha (Rahimahu Allaah) maana ya unayodai. Mimi nayakanusha na siyakubali. Mimi najua kihakika kuwa maneno ya Allaah hayagongani. Aidha najua kuwa maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hayapingani na maneno ya Allaah. Amesema (Ta´ala):

أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ ۚ وَلَوْ كَانَ مِنْ عِندِ غَيْرِ اللَّـهِ لَوَجَدُوا فِيهِ اخْتِلَافًا كَثِيرًا

“Je hawaizingatii Qur-aan? Na lau ingelikuwa imetoka kwa asiyekuwa Allaah, bila shaka wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi.” (04:82)

وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَانًا لِّكُلِّ شَيْءٍ

“Na Tumekuteremshia Kitabu kikiwa ni kielezo bayana cha kila kitu.” (16:89)

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ

“Tumekuteremshia Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao na huenda wakapata kutafakari.” (16:44)

Maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hayapingani na maneno ya Allaah. Vivyo hivyo hakuna mgongano katika maneno ya Allaah. Allaah (Subhaanahu wa Ta´a) ameeleza kuwa hana mshirika na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Uislamu umejengwa juu ya [mambo] matano; kushuhudia ya kwamba hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah… “[1]

Yote haya yanapeana sapoti. Kadhalika yanathibitisha kuwa Allaah hana mshirika katika ´ibaadah kama ambavyo hana mshirika katika uola.

[1] al-Bukhaariy (8) na Muslim (19).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 58-59
  • Imechapishwa: 11/11/2023