214 – Surayj bin Yuunus amenihadithia: Muhammad bin Humayd ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Abu Hayyaan, kutoka kwa Tamiym bin Hadhlam, ambaye amesema:
”Waache na dhahabu na fedha. Kuleni vipande vyenu vya mkate na kunyweni maji yenu ya mto. Wangeliweza, basi wangekufanyeni kukufuru na kukuondosheni.”
215 – Surayj amenihadithia: Muhammad bin Humayd ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Abu Hayyaan, ambaye ameeleza kuwa Abul-´Ubaydayn amesema:
”Ee mja wa Allaah! Wakikuhusuduni kwa mkate wenu mnene, kuleni mkate mwembamba, kunyweni kutoka kwenye mto na shikamaneni barabara na dini yenu.”
216 – Khaalid bin Khidaash ametuhadithia: ´Abdullaah bin Wahb ametuhadithia: ´Amr bin al-Haarith amenikhabarisha kuwa Bukayr bin ´Abdillaah bin al-Ashajj amemuhadithia kuwa ´Umar bin al-Khattwaab alikuwa anasema:
”Pateni bishara! Naapa kwa Allaah! Hakika mimi nataraji mtashiba kwa mkate na mafuta.”
Bi maana dirhamu pana.
217 – Khaalid ametuhadithia: ´Abdullaah bin Wahb ametuhadithia: ´Amr amenikhabarisha kwamba Bukayr bin al-Ashajj amemuhadithia, kutoka kwa ´Atwaa’ bin Yasaar, ambaye amemuhadithia:
”Wanamme wawili kutoka katika Banuu Ghifaar walikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumuomba. Akawaambia: ”Baki hapo mlipo!” Kisha akaondoka na akabaki huko kitambo fulani. Baada ya muda akarudi akiwa na karibu ngumi tatu katika shuka yake ya juu na akasema: ”Hii hapa! Tangu nilipokuacheni nimepambana kwa sababu yenu.”[1]
218 – Abu ´Aliy al-Marwaziy amenihadithia: ´Abdaan bin ´Uthmaan ametukhabarisha: ´Abdullaah ametukhabarisha: Sa´iyd bin Abiy Ayyuub ametukhabarisha: Bakr bin ´Amr amenihadithia, kutoka kwa Swafwaan bin Sulaym, ambaye amesema:
”Watu watafikiwa na kipindi ambapo hamu ya mmoja wao itakuwa tumboni mwake na dini yao itakuwa ni matamanio yao.”
219 – Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: Hishaam bin ´Ubaydillaah ametuhadithia: Yahyaa bin al-´Alaa’ ametuhadithia: Nimefikiwa na khabari kuwa Abu Muslim al-Khawlaaniy amesema:
”Nimeona katika vitabu vya kale jinsi ummah huu utakuwa na watu ambao miungu yao ni matumbo yao na mavazi yao ndio dini yao.”
220 – Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: Zayd al-Khumuriy amenihadithia: Abu ´Abdir-Rahmaan amesema:
”Aakhirah imewashughulisha wenye busara kutokamana na kupika kwenye vyungu na kurekebisha na kuziendekeza ladha.”
221 – Muhammad amesema: Hakiym bin Ja´far amenihadithia: Duwayd Abu Sulaymaan an-Naswibiy amenihadithia, kutoka kwa Shu´ayb bin Maalik bin Yaziyd al-Answaariy, ambaye amesema:
”Ilikuwa inasemwa kwamba njaa ya muda mrefu na kuacha matamanio yanasafisha mwili wa mwanadamu [tupu].”
[1] Kuna swahabah anayekosekana.
- Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 135-139
- Imechapishwa: 31/07/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)