38. Mfumo pekee wa kulingania unaowatengeneza watu

Kwa haya, tunaweza kusema kwa kukata kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewabainishiaUmmah wake njia za kulingania. Ni mamoja kwa maneno au kwa matendo au kwa yote mawili. Ni vipi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atabainisha ada za kukidhi haja lakini asibainishe njia za kulingania ambazo ni muhimu juu ya uwepo wa Uislamu? Kwa vile yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amezibainisha, basi ubainifu wake ndio njia iliowekwa katika Shari´ah ambayo anaongozwa kwayo mpotofu na mwenye kutangatanga. Kwa njia hiyo ndio ambayo amewatoa watu kutoka katika giza na kuwaingiza kwenye nuru. Baadaye njia yake ikafuatwa na Maswahabah watukufu na wale waliowafuata kwa wema. Aidha wakawakemea vikali wale walinganizi wote walioenda kinyume na njia hiyo na wakazua humo. Hakuna jamii kama yao iwezayo kusimama isipokuwa kwa njia hizo zilizosuniwa na za ki-Salaf. Kama alivosema Imaam Maalik (Rahimahu Allaah):

“Mwisho wa Ummah huu hautofaulu isipokuwa yaliyowafanya wa mwanzo wao kufaulu.”

Kuzidisha juu yake ni kuzidisha katika Shari´ah na kutoka nje ya njia ya waumini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayezua katika amri yetu hii kile kisichokuwemokitarudishwa.”[1]

[1] Muslim (1718).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym1
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 46
  • Imechapishwa: 21/05/2023