38. Kupanga safu kuliani na kushotoni mwa imamu

Swali 38: Je, ni jambo limewekwa katika Shari´ah kupanga safu kuliani mwa imamu katika swalah ya jeneza[1]?

Jibu: Haja ikipelekea katika kufanya hivo basi kupangwe safu upande wa kuliani na kushotoni mwake. Sunnah ni kuswali nyuma ya imamu. Lakini ikiwa mahali ni pafinyu hapana neno.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/140).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 31
  • Imechapishwa: 20/12/2021