37. Namna hii Jahmiyyah wanamfananisha Muumba na masanamu

Wakati al-Jahm alipoishiwa na hoja, akakubali kuwa Allaah alimzungumzisha Muusa kikweli, lakini maneno hayakuwa ya Kwake. Tukauliza kama vyengine vyote vimeumbwa isipokuwa Yeye. Akajibu ndio. Tukasema kuwa haya ndio kama yale maneno yao ya kwanza. Isipokuwa mnachotaka nyinyi ni kujilinda na fedha kutokana na yale mnayoyaonyesha. Vilevile az-Zuhriy amesema:

”Wakati Muusa aliposikia maneno ya Mola wake, akasema: ”Ee Mola! Haya ninayoyasikia ni maneno Yako?” Akasema: ”Ndio, ee Muusa, ni maneno Yangu. Nimekuzungumzisha kutokana na nguvu za mwili wako. Ningekuzungumzisha zaidi ya hivyo, basi ungekufa.” Wakati Muusa aliporudi kwa watu wake,wakasema: ”Tueleze maneno ya Mola wako.” Akasema: ”Allaah ametakasika kutokana na mapungufu! Hivi kweli naweza kukuelezeni jambo hilo?” Ndipo wakasema: ”Basi tufananishie.” Akasema: ”Je, mmewahi kusikia mgurumo uliyoambatana na sauti tamu zaidi mliyowahi kusikia? Ni mfano wa hivo.”

Aidha tunawauliza Jahmiyyah ni nani ambaye siku ya Qiyaamah atasema:

يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَـٰهَيْنِ مِن دُونِ اللَّـهِ

“Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Je, wewe uliwaambia watu: “Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu miwili pasi naya Allaah?”[1]

Je, si ni Allaah ndiye atasema hivo? Wakasema kuwa Allaah ataumba kitu ambacho kitaeleza juu ya Allaah, kama ambavo aliumba kitu kikamuongelesha Muusa. Tukawauliza ni nani ambaye amesema:

فَلَنَسْأَلَنَّ الَّذِينَ أُرْسِلَ إِلَيْهِمْ وَلَنَسْأَلَنَّ الْمُرْسَلِينَ فَلَنَقُصَّنَّ عَلَيْهِم بِعِلْمٍ ۖ وَمَا كُنَّا غَائِبِينَ

“Basi bila ya shaka Tutawauliza wale ambao waliopelekewa [Mitume] na tutawauliza Mitume. Kisha Tutawasimulia kwa ujuzi na hatukuwa wenye kukosekana.”[2]

Si ni Allaah ndiye kauliza hivo? Wakasema kuwa haya yote, Allaah ataumba kitu ambacho kitazungumza kwa niaba Yake.

Mmemsemea Allaah uwongo mkubwa mnapodai kuwa haongei. Hivyo mkamfananisha na masanamu yanayoabudiwa badala ya Allaah. Kwa sababu masanamu ndio hayaongei na wala hayatikisiki na wala hayahami kutoka sehemu moja kwenda nyingine[3].

[1] 5:116

[2] 7:6-7

[3] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.” (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 137-138
  • Imechapishwa: 28/04/2024