37. Mtu kufanya kitendo kwa ajili ya dunia ni katika shirki

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

1- Allaah (Ta´ala) amesema:

مَن كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَالَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لاَ يُبْخَسُونَ أُوْلَئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الآخِرَةِ إِلاَّ النَّارُ وَحَبِطَ مَا صَنَعُواْ فِيهَا وَبَاطِلٌ مَّا كَانُواْ يَعْمَلُونَ

”Anayetaka maisha ya dunia na mapambo yake, basi Tutawalipa kikamilifu matendo yao humo nao hawatopunjwa humo; [lakini] hao ndio wale ambao hawatokuwa na chochote katika Aakhirah isipokuwa Moto. Yataharibika yale yote waliyoyafanya humo [hapa duniani] na yatabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.” (Huud 11:15-16)

2- Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ameangamia mja wa dinari! Ameangamia mja wa dirhamu! Ameangamia mja wa Khamiyswah! Ameangamia mja wa Khamiylah! Akipewa huridhia na kama hakupewa hukasirika. Ameangamia na amehiliki mtu huyo! Kama mwiba ukimchoma basi asipate mtu wa kumchomoa! Twuubaa kwa mja ambaye amechukua khitamu za farasi wake kwa ajili ya kupigana Jihaad katika njia ya Allaah; niywele zake ziko timtim na miguu yake imejaa vumbi. Anapowekwa kuchunga [kikosi cha jeshi] basi huchunga kikwelikweli na anapowekwa nyuma kuchunga basi anachunga kikwelikweli. Akiomba idhini asingeliidhinishwa na akiombea basi maombi yake yasingekubaliwa.”[1]

MAELEZO

Shirki imegawanyika katika mafungu mawili; shirki kubwa na shirki ndogo. Shirki iliokusudiwa katika mlango huu wakati fulani inaweza kuwa shirki kubwa na wakati mwingine inaweza kuwa shirki ndogo. Yule mwenye kuingia katika Uislamu kwa sababu ya kutaka manufaa ya kidunia hii  ni shirki kubwa kama wafanyavyo wanafiki ambao watakuwa katika tabaka ya chini kabisa Motoni. Wakati mwingine inakuwa shirki ndogo kama mfano wa yule mwenye kusoma Qur-aan, anaamrisha mema na kukataza maovu kwa kujionyesha. Kadhalika anapigana Jihaad kwa sababu ya ngawira na sio kwa sababu ya Allaah. Huyu ni muumini na muislamu, lakini mambo haya yamemtokea.

1- Allaah (Ta´ala) amesema:

مَن كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَالَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لاَ يُبْخَسُونَ أُوْلَئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الآخِرَةِ إِلاَّ النَّارُ وَحَبِطَ مَا صَنَعُواْ فِيهَا وَبَاطِلٌ مَّا كَانُواْ يَعْمَلُونَ

”Anayetaka maisha ya dunia na mapambo yake, basi Tutawalipa kikamilifu matendo yao humo nao hawatopunjwa humo; [lakini] hao ndio wale ambao hawatokuwa na chochote katika Aakhirah isipokuwa Moto. Yataharibika yale yote waliyoyafanya humo [hapa duniani] na yatabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.”

Haya ni matishio makali. Aayah hii inawahusu makafiri ambao walikuwa wakimwabudu Allaah kwa sababu ya mambo ya kidunia, kama walivokuwa wakifanya wanafiki. Kuenea kwa Aayah kunapelekea kumfanya mtu kutahadhari kufanya ´ibaadah kwa sababu ya manufaa ya kidunia japokuwa hayo yatakuwa katika baadhi ya mambo. Kadhalika Allaah (Ta´ala) amesema:

مَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الْآخِرَةِ نَزِدْ لَهُ فِي حَرْثِهِ وَمَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الدُّنْيَا نُؤتِهِ مِنْهَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِن نَّصِيبٍ

 “Yeyote mwenye kutaka jaza ya Aakhirah basi Tunamzidishia katika jaza yake na yeyote mwenye kutaka jaza ya dunia, tutampa humo, lakini Aakhirah hatokuwa na fungu lolote.” (ash-Shuuraa 42:20)

مَّن كَانَ يُرِيدُ الْعَاجِلَةَ عَجَّلْنَا لَهُ فِيهَا مَا نَشَاء لِمَن نُّرِيدُ ثُمَّ جَعَلْنَا لَهُ جَهَنَّمَ يَصْلاهَا

“Yeyote anayetaka [starehe za dunia] ipitayo upesi, basi Tunamharakizia humo tuyatakayo na kwa tumtakaye – halafu tutamjaalia Jahannam aingie na kuungua hali ya kuwa ni mwenye kutwezwa na ni mwenye kufukuziliwa mbali.” (al-Israa´ 17:18)

Aayah hii imesema kwa kufungamanisha ile iliotangulia kwa sababu sio kila ambaye anaikimbilia dunia huipata. Mtu anaweza kufikia tu baadhi ya yale mambo aliokuwa anatafuta. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَنْ أَرَادَ الآخِرَةَ وَسَعَى لَهَا سَعْيَهَا وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَئِكَ كَانَ سَعْيُهُم مَّشْكُورًا

“Na anayetaka Aakhirah na akaifanyia jitihada vitendo vyake, ilihali ni muumini, basi hao jitihada zao ni za kushukuriwa.” (al-Israa´ 17:19)

Kutaka peke yake hakutoshi pasi na kufanya bidii na imani. Ni lazima kufanya bidii, kumwamini na kumpwekesha Allaah. Bidii ya mtu kama huyu ndio yenye kupendwa na Allaah na waumini. Ni dalili inayofahamisha juu ya uwajibu wa kumtakasia nia Allaah na kwamba kitendo kinabatilika kikichanganyikana pamoja na shirki.

 2- Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ameangamia mja wa dinari! Ameangamia mja wa dirhamu! Ameangamia mja wa Khamiyswah! Ameangamia mja wa Khamiylah! Akipewa huridhia na kama hakupewa hukasirika. Ameangamia na amehiliki mtu huyo! Kama mwiba ukimchoma basi asipate mtu wa kumchomoa! Twuubaa kwa mja ambaye amechukua khitamu za farasi wake kwa ajili ya kupigana Jihaad katika njia ya Allaah; niywele zake ziko timtim na miguu yake imejaa vumbi. Anapowekwa kuchunga [kikosi cha jeshi] basi huchunga kikwelikweli na anapowekwa nyuma kuchunga basi anachunga kikwelikweli. Akiomba idhini asingeliidhinishwa na akiombea basi maombi yake yasingekubaliwa.”

Khamiyswah ni kitambara kilicho na michoromichoro na Khamiylah ni kitambara kilichoshonywa vya watu maarufu na hakina michoromichoro.

Aangamie yule ambaye ameingia katika Uislamu, au anajidhihisha kwa kufanya matendo ya Kiislamu, kwa lengo hili. Aangamie yule ambaye anaabudu kwa ajili ya pesa au mambo ya kidunia. Hivyo ndivo wanavofanya wanafiki na wengineo. Mtu kama huyu anapoteza thawabu zake na badala yake anapata dhambi. Ndio maana (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemuombea du´aa ya maangamivu na kuhiliki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kama mwiba ukimchoma basi asipate mtu wa kumchomoa!”

Huku ni kuomba du´aa dhidi yake asipate mtu wa kumchomoa ili kumfanyia mambo yake mazito na apate mwisho mbaya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Twuubaa kwa mja ambaye amechukua khitamu za farasi wake kwa ajili ya kupigana Jihaad katika njia ya Allaah; niywele zake ziko timtim na miguu yake imejaa vumbi.”

Kutokana na vile anavyoitilia umuhimu na kujishughulisha sana na Jihaad anakosa hata muda wa kuzichanua nywele zake na kuusafisha mwili wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anapowekwa kuchunga [kikosi cha jeshi] basi huchunga kikwelikweli na anapowekwa nyuma kuchunga basi anachunga kikwelikweli. Akiomba idhini asingeliidhinishwa na akiombea basi maombi yake yasingekubaliwa.”

Ni mmoja kati ya watu wengi na hatambuliki. Haya ni kutokana na ukamilifu wa kumtakasia kwake nia Allaah na ukamilifu wa ukweli wake. Hajali nafasi za juu na wala kwenda kwa wafalme, viongozi na nafasi nyenginezo za juu. Ndio maana hawamtambui. Huyu ndiye ana Pepo na karama tofauti na mnafiki na yule mwenye kufanya matendo kwa ajili ya jambo la kidunia wakati anapoamrisha, anapokataza, anapopambana na pindi anapofanya mambo mengine ya kidini; mtu kama huyu matendo yake ni yenye kuporomoka.

[1] al-Bukhaariy (2887).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 120-121
  • Imechapishwa: 27/10/2018