Ukitambua ya kwamba mtu anaweza kukufuru kwa neno analolitoa mdomoni mwake, na pengine amelisema na huku ni mjinga – lakini hapewi udhuru kwa ujinga
MAELEZO
Mtu anaweza kutamka neno la kufuru ambalo likaharibu matendo yake yote kama yule mwanaume aliyesema:
“Ninaapa kwa Allaah ya kwamba hatomsamehe fulani!” Allaah (´Azza wa Jalla) akasema: “Ni nani huyu ambaye anataka kujikweza Kwangu ya kwamba sintomsamehe fulani? Hakika mimi nimemsamehe na nimeyaporomosha matendo yake.”[1]
Neno limoja amefanya ujasiri kwa Allaah na akataka kumkataza Allaah kumsamehe mtenda dhambi huyu. Allaah (´Azza wa Jall) akayaharibu matendo yake na kumghadhibikia.
Mtu anaweza kutamka neno kama hili au mfano wake na akatoka katika Uislamu. Wale waliokuwa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) waliposema: “Hatujaona mfano wa wasomaji wetu hawa! Wana matumbo mapana, wanasema uongo sana na ni waoga wakati wa mapambano.” Wakadai kuwa wamesema hivo kwa sababu ya mzaha na kujiwepesishia uzito na urefu wa safari. Ndipo Allaah akasema juu yao:
قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ
“Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayah Zake na Mtume Wake?” Msitoe udhuru. Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.” [2] (09:65-66)
Ikafahamisha kwamba mwanzoni walikuwa waumini na pindi waliposema maneno haya wakakufuru – Allaah atukinge. Pamoja na kuwa walisema kimzaha tu na kimchezo.
[1] Muslim (2621).
[2] Tazama ”al-Jaamiy´ al-Bayaan fiy Tafsiyr” ya Ibn Jariyr at-Twabariy (01/19-20) na ”Tafsiyr-ul-Qur-aan al-´Adhwiym” ya Ibn Kathiyr (02/351-352).
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 53
- Imechapishwa: 29/11/2016

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 53
Imechapishwa: 29/11/2016
https://firqatunnajia.com/37-mtu-anaweza-kukufuru-kwa-neno-moja-tu-bila-ya-kujua/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)