Hebu tuzingatia namna Allaah alivyowasema kwa ubaya watu wa Kitabu kwa kuwa na moyo msusuwavu baada ya wao kujiliwa na vitabu na wakaziona ishara, ikiwa ni pamoja na kumfufua yule mfu kwa kugusa sehemu ya mwili wa ng´ombe. Hebu tuzingatie namna tulivyokatazwa kujifananisha nao katika hayo. Tukaambiwa:
أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّـهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ
“Je, haujafika wakati kwa walioamini zinyenyekee nyoyo zao kwa ukumbusho wa Allaah na yale yaliyoteremka ya haki, na wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla, ukawarefukia muda, halafu zikawa ngumu nyoyo zao – na wengi miongoni mwao wakatumbukia katika madhambi na kuasi?”[1]
Sababu ya nyoyo zao kuwa susuwavu imebainishwa maeneo mengine:
فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَاقَهُمْ لَعَنَّاهُمْ وَجَعَلْنَا قُلُوبَهُمْ قَاسِيَةًۖ
“Kwa baadaye walivunja ahadi zao, Tuliwalaani na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu.”[2]
Allaah ameeleza kuwa nyoyo zao kuwa ngumu ilikuwa ni adhabu juu yao kwa sababu ya kuvunja ahadi zao. Baada ya Allaah kuchukua fungamano nao, wakaenda kinyume na amri Yake na kuingia ndani ya makatazo Yake. Nasi tukahimizwa kutofanya mfano wake. Kisha baada ya hapo Allaah (Ta´ala) akasema:
يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ ۙوَنَسُوا حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا بِهِ
”Wanayapotosha maneno [Kitabu cha Allaah] kutoka mahali pake na wakasahu sehemu ya yale waliyokumbushwa kwayo.”[3]
Akabainisha kuwa ususuwavu wa nyoyo zao umepelekea katika sifa mbili zenye kusimangwa:
1 – Wanayakengeusha maneno kuyaondosha mahala pake stahiki.
2 – Kusahau sehemu ya yale waliyokumbushwa kwayo. Makusudio ni kuacha na kupuuza ile hekima na mawaidha mema waliyokumbushwa. Hatimaye wakayasahau, wakaacha kuyatendea kazi na kuyapuuzilia mbali.
[1] 57:16
[2] 5:13
[3] 5:13
- Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf, uk. 92-93
- Imechapishwa: 04/10/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
103. Ususuwavu wa moyo sababu yake ni madhambi
Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema: أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّـهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ “Je, haujafika wakati kwa walioamini zinyenyekee nyoyo zao kwa ukumbusho wa Allaah na yale yaliyoteremka ya…
In "7. Sharti ya saba ya jilbaab"
02. Waumini wanamuamini Allaah kwa miili yao, nyoyo zao na ndimi zao
Imani ni maneno na vitendo. Haya yanathibitishwa na Qur-aan na Sunnah. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu kupanda kwa imani: إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا ۚ لَّهُمْ دَرَجَاتٌ عِندَ رَبِّهِمْ…
In "Qurrat-ul-´Aynayn"
38. Nyoyo susuwavu kati ya waislamu
Sifa mbili hizi zinapatikana kwa wale wanazuoni wetu walioharibika wanaofanana na watu wa Kitabu: 1 – Wanayapotosha maneno. Hakika yule ambaye anasoma kwa lengo jengine lisilokuwa matendo moyo wake unakuwa msusuwavu na hivyo matokeo yake hajishughulishi na matendo. Badala yake anakuwa mwenye kukengeusha maneno na kupindisha matamko ya Qur-aan na…
In "Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf"