Kuhusu shubuha ya kutokuwa na uhakika wa yale yanayopokelewa kama madhehebu ya Maswahabah kwa kuwa hayakuandikwa, basi hilo ni dhaifu kuliko nyumba ya buibui. Kwa sababu maneno yetu ni katika yale yaliyopokelewa kutoka kwao katika vitabu vinavyoaminika na vinavyozunguka mikononi mwa watu miongoni mwa vitabu vya Sunnah na Fiqh, khaswa al-Bukhaariy na Muslim. Vimehifadhiwa dhidi ya kuongeza na kupunguza kwa nguvu ya uangalizi juu yake katika ufafanuzi, uhakiki na wingi wa nakala zilizoandikwa kwa mkono zilizo na alama za usikilizaji wa wenye kuhifadhi katika maktabah nyingi – jambo ambalo halipatikani mfano wake katika vitabu vya maimamu wa Fiqh wenye madhehebu mashuhuri. Hapana shaka kwamba hilo ni katika miujiza ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa kuwa Allaah ameweka kwa Sunnah yake watakaoihifadhi kama alivyofanya kwa Ufunuo Wake Mtukufu. Kwake ni sifa zote njema na neema!
Zaidi ya hayo kinachotegemewa tangu uandishi na uainishaji vilipoenea ni kunukuu kutoka katika kilichopo ambacho nafsi inakiamini – ni mamoja kiwe kimekaguliwa chote kwa asili yake au hapana – mradi tu dhana yenye nguvu inaonyesha usahihi wake na moyo unatulia kwa hilo. Hili ndilo linaloitwa kupata (الوجادة). Ndiyo maana Imaam al-Maqbiliy ameraddi katika ”al-´Ilm ash-Shaamikh” juu ya kutokukubali kwao jambo la kupata na kwa kuwa hilo linapingana na matendo yao. Ama uhakika wa kuamini, basi hiyo ni sharti katika kila njia. Bali kutokana na kupata huku ndiko kunakotegemewa na makadhi, watoa fatwa na wanaotoa hukumu, kwa kuwa ni vigumu kuunganisha kila kitabu na mtunzi wake kwa cheni ya wapokezi na kukithibitisha kutoka kwake kwa kusikia na kusoma katika tabaka zote. Pamoja na hayo vitabu vya Hadiyth vimepatikana ndani yake uhakiki, upokeaji, maelezo yake na kuhesabiwa kwa nakala zake zilizosahihishwa kwa kujivunia kusomwa kwake na kujipatia heshima kwa kusikilizwa kwake, kupokelewa kwake na kupewa idhini yake, jambo ambalo halipatikani hata sehemu ya kumi ya kumi yake katika maandiko ya maimamu wanne wala wengineo. Lau ingetakiwa kunakili kitabu katika maandiko ya maimamu au kukichapisha, basi kingekabiliwa na vikwazo vya kukosa nakala kamili[1], kama vinavyojulikana. Mara nyingi baada ya uchunguzi haupatikani isipokuwa vipande vilivyotawanyika au nakala iliyopungua, ilihali haki ya wanaowafuata maimamu wao ni kunakili kutoka humo katika kila karne maelfu ya nakala na kuvihudumia kwa kusoma, kufundisha, kusambaza na kuvitolea maelezo.
Nilijitahidi mara moja kupata nakala iliyoandikwa kwa mkono ya kitabu ”al-Umm” au maelezo yake ili niilinganishe na iliyochapishwa na ninakili maelezo – lakini sikupata nakala yake katika maktabah yoyote miongoni mwa maktabah za Shaam nzima. Hili likoje likilinganishwa na nakala za vitabu vya al-Bukhaariy, Muslim, vitabu vyenginee vya Hadiyth zilizoandikwa kwa mkono ambazo maktabah za dunia zimejaa. Si vigumu kwa mwanafunzi kupata zilizo bora miongoni mwazo. Je, kuamini vitabu vya Sunnah, na yale masimulizi yao na fatwa zao kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ya Maswahabah, si yenye kuaminika zaidi kuliko vyengine vyote? Ndio, bila shaka.
[1] Hiki ndio kilichotokea wakati wa kuchapishwa ”al-Umm” ya ash-Shaafi´iy; walilazimika kukusanya pande zake mbalimbali kutoka nchi mbalimbali. Wakakilinganisha na vitabu vingine vyote.
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 59-90
- Imechapishwa: 14/04/2026

Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 59-90
Imechapishwa: 14/04/2026
https://firqatunnajia.com/36-vitabu-vya-hadiyth-vitabu-ulimwenguni-vinavyoaminika-zaidi/