35. Ikiwa umelazimika kumfuata mtu kichwa mchunga

Maandiko kuhusu kuzingatia maneno ya Maswahabah ni mengi mno kiasi cha kwamba hayawezi kuhesabiwa. Tunasema haya kama utangulizi wa maneno yaliyopokelewa kuhusu kupaka juu ya soksi kwa Abu Daawuud na wengineo, kwani hayo ni hoja katika mlango huu kwa kila atakayepinga, vyovyote itakavyokuwa hali yake. Kwa sababu, kwa mujibu wa ufafanuzi wa Ibn Taymiyyah na walivyothibitisha wanazuoni wa misingi, ima yamesambaa bila kukanushwa – na yaliyo hivyo ni hoja kwa maafikiano – au yamesemwa na baadhi yao bila kusambaa kauli ya kuyapinga – na jopo la wanazuoni wanalijengea hoja. Imejulikana kwamba hapana mpinzani aliyesambaza maoni yake, kwa kuwa hakukupokelewa kutoka kwao katika hilo isipokuwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au wao wenyewe walifanyia kazi kitendo hicho. Ni jambo liko wazi kabisa katika mlango wa hukumu kwamba hukumu ambayo imefikia idadi ya wapokezi wake, wenye kuikubali na wenye kuifanyia kazi kuwa kumi na sita, lau wangekuwa si katika daraja ya Maswahabah, isingesita kukubaliwa. Basi tusemeje hali ikiwa wote ni katika daraja ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum)? Haya yote ni kwa dhana kwamba haikupokelewa katika mlango huu wa kupaka juu ya soksi isipokuwa maneno yao tu. Vinginevyo tumetanguliza yale yaliyopokelewa katika hilo miongoni mwa Hadiyth ambazo ndizo hoja katika mlango huu na ndizo marejeo wakati wa makinzano: “Unapokuja Mto wa Allaah basi hubatilika mto wa Ma´qal.” Hakika jumla hii inapaswa kuzingatiwa na wale wasiotaka isipokuwa kufuata kichwa mchunga ili wajue kwamba mwenye kuchagua kufuata kichwa mchunga, basi lililo bora kwake ni kuwafata kichwa mchunga Maswahabah kwa kuwa wao ni wenye elimu zaidi. Wanazuoni wa misingi wameafikiana kwamba hutangulizwa mbele – katika mlango wa kufuata kichwa mchunga – aliye mjuzi zaidi. Ibn-ul-Qayyim katika ”I´laam-ul-Muwaqqi´iyn”:

”Haijulikani ni udhuru gani alionao mwenye kufuata kibubusa katika kutanguliza mbele maneno ya wasiokuwa Maswahabah juu ya maneno yao, basi vipi ikiwa atazuia kuchukua maneno ya Swahabah, basi vipi ikiwa ataanza kumtuhumu Bid´ah yule mwenye kufanyia kazi maneno yao?  Hapana shaka kwamba amechukua methali inayotambulika ”Usirushie wengine mawe ikiwa nyumba yako ni ya vioo”.”

  • Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 57-59
  • Imechapishwa: 14/04/2026