Ukifahamu hili basi itakubainikia kwamba yaliyokuja katika ”Jam´-ul-Jawaami´” cha as-Subkiy ya kwamba kuna mitazamo miwili tofauti kuhusu kumfuata kibubusa Swahabah, ambapo ya kwanza ni katazo kwa madai ya kuondoka kwa uaminifu wa madhehebu yake kwa kuwa hayakuandikwa; mfasiri wake akalihusisha hilo na Imaam al-Haramayn al-Juwayniy na wahakiki wengine (yaani wanaomfuata kibubusa al-Juwayniy na wafuasi wake). Hayo ni maneno ya kijumla ambayo asiwepo yeyote mwenye kughurika na udhahiri wake. Maimamu wengi wanayarudisha – bali as-Subkiy mwenyewe aliyarudisha. az-Zarakshiy amemnukuu kwamba amesema:
”Ikiwa imethibiti kwa yakini madhehebu yake, basi kufuata kibubusa madhehebu yake kunajuzu kwa maafikiano.”
Kwa maana maneno ya Swahabah.
Wakati al-´Izz bin ´Abdis-Salaam aliulizwa kuhusu mtu ambaye imethibiti kwake madhehebu ya Abu Bakr au mmoja wa wanazuoni wa Maswahabah katika jambo fulani, je, aruhusiwe kuacha na kufuata mwingine au hapana, akajibu ifuatavyo:
”Ikiwa imethibiti kutoka kwa mmoja wa Maswahabah madhehebu katika hukumu miongoni mwa hukumu, basi haijuzu kuiacha isipokuwa kwa dalili iliyo wazi zaidi kuliko dalili yake…. Si wajibu kwa wanazuoni wanaojitahidi kuwafuata Swahabah katika masuala yenye maoni tofauti, bali hilo halihalali pale dalili zao zinapokuwa wazi zaidi kuliko dalili za Maswahabah.”
Ibn Taymiyyah amesema:
”Ama maneno ya Maswahabah, ikiwa yamesambaa na hayakukanushwa katika zama zao, basi hayo ni hoja kwa wanazuoni wengi. Ikiwa walikhitalifiana, basi yale waliyokhitalifiana hurejeshwa kwa Allaah na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na halikuwa neno la mmoja wao kuwa hoja pamoja na kupingwa na mwenzake kwa maafikiano ya wanazuoni. Ikiwa baadhi yao amesema neno na wengine hawakusema kinyume chake na wala halikusambaa, basi katika hilo kuna makinzano. Wanazuoni wengi, kama Abu Haniyfah, Maalik, Ahmad katika riwaya mashuhuri kutoka kwake na ash-Shaafi´iy katika moja ya maoni yake, hulijengea hoja.”
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 56-57
- Imechapishwa: 14/04/2026

Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 56-57
Imechapishwa: 14/04/2026
https://firqatunnajia.com/34-haijuzu-kuacha-maneno-ya-maswahabah/