Maneno na fatwa za Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) zina haki zaidi kuchukuliwa kuliko wengine na majibu kwa anayodai kuondoka kwa uaminifu wa yaliyopokelewa kutoka kwao. Huu ni utafiti mkubwa. Ni wajibu kwa kila aliyeonja hata sehemu ndogo ya elimu ausikilize kwa makini. Hilo ni kwa sababu watu wengi anapotajwa mbele yao msimamo wa Swahabah katika suala fulani, humuoni akilipa umuhimu hata kidogo. Wakitegemea kuwa si miongoni mwa waliolazimishwa kufuatwa. Huenda akaenda mbali zaidi na akasema kwamba hakuna aliyeandika madhehebu yake.
Kwa kuwa hili si jambo dogo katika dini, kwa kuwa kauli kama hiyo ni yenye kukataliwa kwa wale waliobobea katika elimu, ndipo ikalazimu kuondoa mkanganyiko huu kwa kuwaongoza wachamungu. Hilo ni kwa sababu Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) wako katika daraja ya juu kabisa na nafasi tukufu zaidi katika kila elimu, kila tendo, katika fadhilah na heshima. Imaam Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema katika ”I´laam-ul-Muwaqqi´iyn”:
”Kama ambavyo Maswahabah ni mabwana wa ummah, maimamu wake na viongozi wake basi ndivyo walivyo mabwana wa watoa fatwa na wanazuoni.” Mujaahid amesema: ”Wanazuoni ni Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”
Akanukuu (Rahimahu Allaah) kutoka kwa ash-Shaafi´iy kwamba alisema kuhusu Maswahabah:
”Wao wako juu yetu katika kila elimu, ijtihadi, uchamungu, akili na kila jambo ambalo kwa hilo elimu hupatikana upya. Maoni yao kwetu ni bora zaidi na yanastahiki zaidi kwetu kuliko maoni yetu wenyewe.”
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 55
- Imechapishwa: 14/04/2026
Maneno na fatwa za Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) zina haki zaidi kuchukuliwa kuliko wengine na majibu kwa anayodai kuondoka kwa uaminifu wa yaliyopokelewa kutoka kwao. Huu ni utafiti mkubwa. Ni wajibu kwa kila aliyeonja hata sehemu ndogo ya elimu ausikilize kwa makini. Hilo ni kwa sababu watu wengi anapotajwa mbele yao msimamo wa Swahabah katika suala fulani, humuoni akilipa umuhimu hata kidogo. Wakitegemea kuwa si miongoni mwa waliolazimishwa kufuatwa. Huenda akaenda mbali zaidi na akasema kwamba hakuna aliyeandika madhehebu yake.
Kwa kuwa hili si jambo dogo katika dini, kwa kuwa kauli kama hiyo ni yenye kukataliwa kwa wale waliobobea katika elimu, ndipo ikalazimu kuondoa mkanganyiko huu kwa kuwaongoza wachamungu. Hilo ni kwa sababu Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) wako katika daraja ya juu kabisa na nafasi tukufu zaidi katika kila elimu, kila tendo, katika fadhilah na heshima. Imaam Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema katika ”I´laam-ul-Muwaqqi´iyn”:
”Kama ambavyo Maswahabah ni mabwana wa ummah, maimamu wake na viongozi wake basi ndivyo walivyo mabwana wa watoa fatwa na wanazuoni.” Mujaahid amesema: ”Wanazuoni ni Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”
Akanukuu (Rahimahu Allaah) kutoka kwa ash-Shaafi´iy kwamba alisema kuhusu Maswahabah:
”Wao wako juu yetu katika kila elimu, ijtihadi, uchamungu, akili na kila jambo ambalo kwa hilo elimu hupatikana upya. Maoni yao kwetu ni bora zaidi na yanastahiki zaidi kwetu kuliko maoni yetu wenyewe.”
Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 55
Imechapishwa: 14/04/2026
https://firqatunnajia.com/33-maoni-na-fatwa-za-maswahabah-vina-nguvu-zaidi/