Swali: Mtu anaswali peke yake baadaye akaja mtu na kujiunga naye na yule mtu wa kwanza akamswalisha. Je, swalah inasihi?
Jibu: Ndio, ni sahihi. Dalili ya hilo ya hilo ni yale yaliyothibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwamba
“Alilala kwa shangazi yake Maymuunah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasimama kuswali usiku. Ndipo akaja Ibn ´Abbaas na kujiunga naye na akaendelea katika swalah yake.”[1]
Haya yalitokea katika swalah ya usiku – na yale yanayofaa katika swalah inayopendeza yanafaa pia katika swalah ya faradhi isipokuwa kwa dalili inayoonyesha kinyume. Katika suala hili hakuna dalili inayotofautiana swalah inayopendeza na swalah ya faradhi. Bali Imaam Ahmad amepokea kwamba Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisimama kuswali Maghrib, nikaja na kusimama kushotoni mwake ambapo akaniweka kuliani mwake.”[2]
Hii ilikuwa ni katika swalah ya faradhi.
Baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa kitendo hicho hakisihi si katika faradhi wala swalah ya kujitolea, na ndio maoni yanayotangaa katika madhehebu. Imesemekana vilevile ya kwamba inasihi katika swalah ya kujitolea pasi na swalah ya faradhi.
1387-2-24
[1] al-Bukhaariy (697).
[2] Ahmad (3/326) na Ibn Maajah (974). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (801).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/445-446)
- Imechapishwa: 14/04/2026
Swali: Mtu anaswali peke yake baadaye akaja mtu na kujiunga naye na yule mtu wa kwanza akamswalisha. Je, swalah inasihi?
Jibu: Ndio, ni sahihi. Dalili ya hilo ya hilo ni yale yaliyothibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwamba
“Alilala kwa shangazi yake Maymuunah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasimama kuswali usiku. Ndipo akaja Ibn ´Abbaas na kujiunga naye na akaendelea katika swalah yake.”[1]
Haya yalitokea katika swalah ya usiku – na yale yanayofaa katika swalah inayopendeza yanafaa pia katika swalah ya faradhi isipokuwa kwa dalili inayoonyesha kinyume. Katika suala hili hakuna dalili inayotofautiana swalah inayopendeza na swalah ya faradhi. Bali Imaam Ahmad amepokea kwamba Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisimama kuswali Maghrib, nikaja na kusimama kushotoni mwake ambapo akaniweka kuliani mwake.”[2]
Hii ilikuwa ni katika swalah ya faradhi.
Baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa kitendo hicho hakisihi si katika faradhi wala swalah ya kujitolea, na ndio maoni yanayotangaa katika madhehebu. Imesemekana vilevile ya kwamba inasihi katika swalah ya kujitolea pasi na swalah ya faradhi.
1387-2-24
[1] al-Bukhaariy (697).
[2] Ahmad (3/326) na Ibn Maajah (974). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (801).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/445-446)
Imechapishwa: 14/04/2026
https://firqatunnajia.com/anayeswali-peke-yake-kuwa-imamu/