Swali: Ni ipi hukumu ya Uislamu kuhusu maneno ya Shaykh Muhammad ‘Abduh ya kuhalalisha ribaa na kufuta ndoa ya wake wengi?
Jibu: Kuhalalisha ribaa ni jambo zito sana. Hakuna anayehahalalisha ribaa isipokuwa kafiri. Lakini nani kasema kwamba yeye amehahalalisha ribaa? Nani kasema kwamba amekataza ndoa ya wake wengi? Hili linahitaji kurejewa katika vitabu vyake. Sisi hatujishughulishi na watu binafsi, tunashughulika na hukumu ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Watu wote hukosea na hupatia, isipokuwa yule Allaah aliyemlinda na kumuepusha. Wanadamu wote hukumbwa na makosa.
Muhammad ´Abduh ana makosa yake na wengine pia wana makosa yao. Lakini hoja kuu ni kwamba ribaa kamwe haiwezi kuhalalishwa na mtu yeyote. Anayehahalalisha ribaa kwa makusudi, huku akijua iko haramu, halafu akaifanya halali kwa ukaidi na kwenda kinyume na amri ya Allaah, huyo ni kafiri. Ni sawa na yule anayehahalalisha uzinzi au pombe, naye huwa kafiri. Lakini mtu akifanya Ijtihaad na akachanganyikiwa katika baadhi ya aina za ribaa huku akadhani kuwa ni halali kwa sababu fulani, yeye ana hukumu ya wenye kujitahidi. Akipatia hupata thawabu mbili na akipotea hupata thawabu moja.
Kuhusu ndoa ya wake wengi, watu wengi miongoni mwa waandishi wa kimagharibi – manaswara, mayahudi na wengine – wameandika wakilalamikia ukewenza katika Uislamu. Wao ndio waliokosea, ndio wanaopinga na ndio waliopotea. Wengi wao wanajua ukweli, lakini ni ukaidi, hasadi na dhuluma. Vinginevyo wengi wameshathibitisha kuwa ukewenza uliohalalishwa na Shari´ah ndio haki na ndio tiba ya matatizo ya kijamii. Waandishi wao wa haki, wanaume kwa wanawake, wamekiri ya kwamba yale yaliyoletwa na Uislamu katika kuoa wake wengi ndio ni njia sahihi ya kuokoa jamii kutokana na maanguko ya maadili. Lakini baadhi yao wanapinga kwa sababu ya kuwaogopa viongozi wao kutokana na maslahi yao binafsi au kwa chuki dhidi ya waislamu. Cha kushangaza wengi wa hawa wanaosema ukewenza ni uovu, wao wanaoa mke mmoja lakini wanashirikiana kimapenzi na makumi ya wanawake nje ya ndoa. Kwa hivyo kuna tofauti gani? Muislamu anachukua wake halali wawili, watatu au wanne kwa idhini ya Shari´ah. Akiwa mwenye uadilifu, basi yuko katika kheri kubwa. Lakini hawa wanaopinga Uislamu wanachukua wanawake wa zinaa bila idadi. Hii ni tabia mbaya na yenye maovu mengi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1173/الرد-على-من-يحل-الربا-ويمنع-تعدد-الزوجات
- Imechapishwa: 14/04/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1173/الرد-على-من-يحل-الربا-ويمنع-تعدد-الزوجات
Imechapishwa: 14/04/2026
https://firqatunnajia.com/hali-ya-wengi-wanaopinga-kuoa-mke-zaidi-ya-mmoja/