Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

1- Allaah (Ta´ala):

قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَى إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَهُكُمْ إِلَهٌ وَاحِدٌ فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاء رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا

”Sema: “Hakika mimi ni mtu [wa kawaida] kama nyinyi. Nafunuliwa Wahy kwamba hakika mwabudiwa wenu wa haki ni Mungu mmoja pekee. Hivyo yule anayetaraji kukutana na Mola wake basi na atende matendo mema na wala asimshirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote!” (al-Kahf 18:110)

2- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Ta´ala) amesema: “Hakika Mimi ni Mwenye kujitosheleza kutohitajia washirika. Hivyo basi yule atakayefanya kitendo akanishirikisha Mimi pamoja na mwingine, basi nitamwacha yeye na shirki yake.”[1]

Ameipokea Muslim.

3- Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Je, nisikwambieni kile ninachokukhofieni kuliko hata huyo al-Masiyh ad-Dajjaal?” Wakasema: “Ndio.” Akasema: “Ni shirki iliyojificha; anasimama mtu kuswali na akaipamba swalah yake kwa kuwa anaona watu wanamwangalia.”[2]

Ameipokea Ahmad.

MAELEZO

Mtunzi wa kitabu ameweka mlango huu ili kutahadharisho kujionyesha. Kujionyesha maana yake ni mtu kufanya kitendo ili wengine wapate kumuona au kumsifu au ili aweze kufikia kitu cha kimanufaa cha kidunia. Inaweza vilevile kutaka kuwafanya wengine wamsikie namna anavyosoma Qur-aan, namna  anavyomsabihi Allaah, namna anavyoamrisha mema na kukataza maovu. Kwa ajili hiyo imekuja katika Hadiyth:

“Yule anayetaka kujionyesha basi Allaah atamfanya kuonekana na yule anayetaka kusikika basi Allaah atamfanya kusikika.”[3]

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Yule anayetaka kujionyesha basi Allaah atamuonyesha na yule anayetaka kusikika basi Allaah atamfanya kusikika.”

Bi maana atamfedhehesha na atamlipa kwa mujibu wa kitendo chake. Ni wajibu kwa muislamu kumtakasia matendo yake Allaah na kutarajia thawabu kutoka kwa Allaah.

 1- Allaah (Ta´ala):

قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَى إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَهُكُمْ إِلَهٌ وَاحِدٌ فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاء رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا

”Sema: “Hakika mimi ni mtu [wa kawaida] kama nyinyi. Nafunuliwa Wahy kwamba hakika mwabudiwa wenu wa haki ni Mungu mmoja pekee. Hivyo yule anayetaraji kukutana na Mola wake basi na atende matendo mema na wala asimshirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote!”

Tendo jema ni lile lililotimiza masharti mawili:

1- Kumtakasia nia Allaah katika ´ibaadah zote.

2- Kiwe kimeafikiana na Shari´ah na kisiwe kimezuliwa.

Yule ambaye kweli anataraji kukutana na Mola wake basi afanye matendo mema yenye kuafikiana na Shari´ah na asimshirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote.

2- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Ta´ala) amesema: “Hakika Mimi ni Mwenye kujitosheleza kutohitajia washirika. Hivyo basi yule atakayefanya kitendo akanishirikisha Mimi pamoja na mwingine, basi nitamwacha yeye na shirki yake.”

Ameipokea Muslim.

Haya yanafahamisha kwamba Allaah anajitenga mbali na kitendo ambacho ndani yake kina shirki na kwamba hayakubali. Katika upokezi mwingine imekuja:

“Mimi ni Mwenye kujitenga nayo mbali. Bali ni ya yule aliyemshirikisha.”

Hii ni dalili inayofahamisha juu ya uwajibu wa kumtakasia matendo Allaah.

3- Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Je, nisikwambieni kile ninachokukhofieni kuliko hata huyo al-Masiyh ad-Dajjaal?” Wakasema: “Ndio.” Akasema: “Ni shirki iliyojificha; anasimama mtu kuswali na akaipamba swalah yake kwa kuwa anaona watu wanamwangalia.”

Siku ya Qiyaamah Allaah atawaambia wale waliojionyesha:

“Allaah atawaambia wale waliojionyesha: “Nendeni kwa wale mliokuwa mkiwaonyesha duniani na muone kama watakulipeni.”

Haya yanaonyesha ukhatari wa kujionyesha na khaswakhaswa kwa wale wafanya ´ibaadah. Yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwakhofia Maswahabah ilihali ndio watu bora kabisa. Kwa sababu jambo la kujionyesha linawatokea wema. Wanapewa majaribio ya kujionyesha kama  wanavyopewa majaribio wengine na wanalichukulia hilo wepesi. ad-Dajjaal mtu anaweza kumtambua kutokana na zile alama. Shirki iliyojificha ni khatari kwa sababu imefichikana moyoni mwa mwanadamu. Lakini ina baadhi ya ishara ambazo zinaweza kuonekana kwa mwenye nayo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kama ilivyosihi kutoka kwake:

“Kikubwa ninachokikhofieni juu yenu ni shirki ndogo.” Alipoulizwa juu yake akasema: “Kujionyesha.”[4]

[1] Muslim (2985).

[2] Ahmad (11270) na Ibn Maajah (4203). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (3389).

[3] al-Bukhaariy (6499) na Muslim (93).

[4] Ahmad (23680). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaami´” (1555).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 118-119
  • Imechapishwa: 24/10/2018