34. Mlango kuhusu maneno Yake (Ta´ala) “Je, wameaminisha na mipango ya Allaah? Basi hawaaminishi mipango ya Allaah isipokuwa watu wenye kukhasirika.”

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

1-

Allaah (Ta´ala) amesema:

أَفَأَمِنُوا مَكْرَ اللَّـهِ ۚ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ

”Je, wameaminisha na mipango ya Allaah? Basi hawaaminishi mipango ya Allaah isipokuwa watu wenye kukhasirika.” (al-A´raaf 07:99)

2-

وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِ إِلَّا الضَّالُّونَ

“Na nani anayekata tamaa na rehema ya Mola wake isipokuwa waliopotea.” (al-Hijr 15:56)

3- Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kwamb Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusiana na madhambi makubwa halafu ambapo akajibu:

“Kumshirikisha Allaah, kukata tamaa na rehema ya Allaah na kujiaminisha na mipango/njama za Allaah.”[1]

4- Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Madhambi makubwa kabisa ni kumshirikisha Allaah, kujiaminisha mipango/njama za Allaah, kukata tamaa na rehema ya Allaah na kukata tamaa na rafaja ya Allaah.”[2]

Ameipokea ´Abdur-Razzaaq.

MAELEZO

1-

Allaah (Ta´ala) amesema:

أَفَأَمِنُوا مَكْرَ اللَّـهِ ۚ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ

”Je, wameaminisha na mipango ya Allaah? Basi hawaaminishi mipango ya Allaah isipokuwa watu wenye kukhasirika.”

2-

وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِ إِلَّا الضَّالُّونَ

“Na nani anayekata tamaa na rehema ya Mola wake isipokuwa waliopotea.”

Mlango huu unazumgumzia kwamba ni haramu kujiaminisha na njama za Allaah, kukatika moyo na rehema ya Allaah na baadhi ya madhambi mengine makubwa. Kujiaminisha na njama za Allaah ni dhambi kubwa na ni jambo linapelekea mtu kuchukulia wepesi na maharamisho ya Allaah. Kwa sababu yule ambaye atajiaminisha na njama za Allaah basi matendo yake, tabia yake na mienendo yake itakuwa miovu na hatomcha Allaah.

Kukata tamaa na faraja ya Allaah ndio kukata tamaa na rehema ya Allaah. Kutaka tamaa na faraja ya Allaah ni kumdhania vibaya Allaah na kuvunjika moyo. Muislamu anapaswa awe kati na kati;  anatakiwa kutarajia rehema ya Allaah na kuogopa kwa sababu ya madhambi yake. Asizame katika maasi na akajiaminisha na njama za Allaah. Vilevile hatakiwi kukata tamaa na rehema ya Allaah. Anatakiwa awe kama ndege na mbawa mbili. Baadhi ya wanachuoni wamependekeza kuwa na khofu zaidi wakati mtu yuko na afya njema, kwa sababu ambaye ana afya njema ana uwezo mkubwa wa kutendea kazi maasi, na kuwa na matarajio zaidi wakati wa ugonjwa, kwa sababu mgonjwa ni mdhaifu wa kufanya matendo mema. Msingi ni kwamba anatakiwa awe kati na kati kwa hayo mawili.

3- Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kwamb Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusiana na madhambi makubwa halafu ambapo akajibu:

“Kumshirikisha Allaah, kukata tamaa na rehema ya Allaah na kujiaminisha na mipango/njama za Allaah.”

Haya yamepokelewa kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kutoka kwa Swahabah. Hata kama yamesemwa na Swahabah, yana hukumu moja kama maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sababu hawezi kusema hivo kutoka kichwani mwake mwenyewe. Inawezekana vilevile kayasema Ibn ´Abbaas kutoka kichwani mwake mwenyewe kwa kutegemea dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Kwa hali yoyote ile ni maneno sahihi.

 4- Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Madhambi makubwa kabisa ni kumshirikisha Allaah, kujiaminisha mipango/njama za Allaah, kukata tamaa na rehema ya Allaah na kukata tamaa na rafaja ya Allaah.”

Ameipokea ´Abdur-Razzaaq.

Shirki ndio dhambi kubwa kabisa kwa sababu inaporomosha matendo mengine yote. Vilevile kuvunjika moyo na faraja ya Allaah, ambako ni kule kukata tamaa kwa kiasi kikubwa, ni dhambi kubwa. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِ إِلَّا الضَّالُّونَ

“Na nani anayekata tamaa na rehema ya Mola wake isipokuwa waliopotea.”

Hili ni swali limeulizwa kwa njia ya makanusho. Bi maana hii ni sifa ya wapotevu peke yao.

Ama kuhusu madhambi makubwa mengine yote, hayaporomoshi matendo mema.

[1] Majma´-uz-Zawaa-id (1/104).

[2] Majma´-uz-Zawaa-id (1/104).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 113-114
  • Imechapishwa: 24/10/2018