36. Kufupisha na kukusanya kwa anayefanya kazi ya wanamaji

Swali 36: Mimi ni mtu ninayefanya kazi katika jeshi la wanamaji na mabaharia na tunasafiri kwa meli kutoka bandarini hadi baharini kwa muda wa siku tatu au nne. Je, inafaa kufupisha swalah na kuzikusanya pamoja na kuzingatia kwamba kupanda kwetu juu hakuko mbali sana na mji, isipokuwa hayo yanafanyika katika baadhi ya kazi[1].

Jibu: Abiria wa meli au abiria wa aina nyingine za marikebu za baharini, kwa mfano wa abiria wa gari na treni nchikavu, ikiwa masafa ni yale yanayokubalika kufupisha basi atafupisha na kukusanya. Vinginevyo hapana. Iwapo meli iko karibu na bandari au karibu na pwani na haiendi mbali, kama vile umbali wa 10 km, 20 km au mfano wa hivo, basi huyu haifai kwake kufupisha na wala hana hukumu ya safari. Lakini ikiwa inaenda maeneo ya mbali yanayozingatiwa kuwa ni safari, kwa mfano 70 km, 80 km, 100 km au zaidi ya hapo, basi hii inazingatiwa ni safari. Watu wake wanaruhusiwa kufupisha na kukusanya kati ya swalah mbili. Kwa sababu ni wasafiri. Ni kama mfano wa wale ambao wanatoka kwenda nyikani kwa ajili ya pikniki au mfano wake kwa umbali wa 80 km, 70 km, 90 km, 100 km au yaliyo zaidi ya hivo.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/279).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 52-53
  • Imechapishwa: 05/05/2022