36. Kufanya safu nyingi ijapo za mbele hazijakamilika

Swali 36: Ni ipi hukumu kuhusiana na jambo la kufanya safu nyingi ingawa haijakamilika safu ya kwanza[1]?

Jibu: Msingi ni kwamba safu katika swalah ya jeneza zipangwe kama zinavyopangwa katika swalah za faradhi. Safu za mwanzo ndizo zianze kukamilishwa. Ama kitendo cha Maalik bin Hubayrah (Radhiya Allaahu ´anh) katika cheni ya wapokezi wake kuna unyonge. Isitoshe inaenda kinyume na Hadiyth Swahiyh ambazo zinajulisha juu ya ulazima wa kukamilisha safu za mwanzo katika swalah.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/139).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 30
  • Imechapishwa: 19/12/2021