Swali 37: Imamu anasimama vipi katika swalah ya jeneza[1]?

Jibu: Ni katika Sunnah imamu kusimama usawa na kichwa cha mwanamme na usawa wa katikati na mwanamke. Majeneza yakiwa mengi anatangulizwa mbele mwanamme, kisha mtoto wa kiume, kisha mwanamke, kisha mtoto wa kike na anaswalia wote. Lengo ni kuliharakisha jeneza. Kichwa cha mtoto wa kiume kiwekwe usawa na kichwa cha mwanamme na katikati ya mwanamke usawa na kichwa cha mwanamme na vivyo hivyo mtoto wa kike kwa ajili ya kutendea kazi Sunnah.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/139).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 30-31
  • Imechapishwa: 19/12/2021