35. Ubora wa maiti kuswaliwa na watu wengi

Swali 35: Je, kuna fadhilah juu ya wingi wa idadi ya wenye kumswalia maiti[1]?

Jibu: Imethibiti katika Hadiyth ya Ibn ´Abbaas ambaye amesimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:

“Hakuna mtu yeyote katika waislamu anayekufa wakasimama katika jeneza lake watu arobaini ambao hawamshirikishi Allaah na chochote isipokuwa Allaah atawakubalia maombezi yao kwa ajili yake.”[2]

Ameipokea Muslim.

Kwa ajili hiyo wanazuoni wamependekeza kuchagua msikiti ambao kuna kikosi cha watu wengi ili kumswalia maiti mahali hapo. Kila ambavo idadi ni kubwa ndivo inavokuwa karibu zaidi na kheri na kuombewa du´aa kwa wingi.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/138).

[2] Ahmad (2505) na Muslim (948).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 29-30
  • Imechapishwa: 19/12/2021