Ni vipi mtu ambaye moyoni mwake mna imani na hekima ndogo kabisa anaweza kufikiria kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuibainishia mada hii kikamilifu kabisa? Hebu tuseme kuwa hakufanya hivo; ni jambo la muhali watu bora wa Ummah wake na karne bora hawakufanya hivo kwa njia moja au nyingine.

MAELEZO

Ni vipi mtu ambaye ana chembe kidogo kabisa ya akili anaweza kufikiria kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipuuza suala hili na hakuwabainishia nalo watu mpaka walipokuja kizazi cha Jahmiyyah ndipo wakawabainishia watu na sambamba na hilo wakawatia upotofuni Salaf au wakawatuhumu ujinga na kwamba hawajui lolote? Dhana hii haiwezekani kwa sababu mbili:

1 – Haiwezekani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliacha kubainisha suala hili. Na ikiwa yeye hakulibainisha, ni kitu gani alichobainisha? Yule mwenye kuona kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakubainisha jambo hilo ni kafiri.

2 – Haiwezekani ikawa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alibainisha jambo hili ambapo Maswahabah wakalificha na wasilinukuu na wasiwabainishie watu. Wao ndio viumbe bora, vizazi bora, viumbe wanaowatakia watu mema zaidi na viumbe wajuzi zaidi baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maswahabah ndio wajumbe kati yetu sisi na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Dini hii haikutufikia isipokuwa kupitia wao. Wao ndio ambao wametufikishia Qur-aan. Baada ya wao kujifunza nayo kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakatufunza nayo. Wao ndio ambao wametufikishia Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wametusimulia Hadiyth moja baada ya nyingine. Hakuna Hadiyth yoyote isipokuwa imepokelewa na Maswahabah wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 66-67
  • Imechapishwa: 04/08/2024