Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Bali utambuzi huu ndio kiini cha Da´wah ya Mitume na ujumbe wa kiungu.

MAELEZO

Tawhiyd ndio kiini cha ulinganizi wa Mitume, khaswa Mtume wa mwisho na kiongozi wa Mitume wote, naye si mwingine ni Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ulinganizi huo unahusiana na kumtambua Allaah na kumwabudu na kumfikia. Hilo ndio lilikuwa lengo la ulinganizi wa Mitume wote. Mengine yote ni njia. Kila Mtume alikuwa akiwaambia watu wake:

يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ

“Enyi watu wangu! Mwabuduni Allaah, kwani hakika hamna mungu wa haki asiyekuwa Yake.”[1]

Namna hii ndio ulikuwa ujumbe wa Mtume. Walilingania katika hilo na wakaamirisha hilo. Ni vipi tutamwabudu Allaah ilihali hatuamini majina na sifa Zake? Haliwezekani hili. Ikiwa hatuamini majina na sifa Zake hatujui haki na ukubwa Wake. Sisi hatujamuona kwa macho, lakini tunamtambua kupitia majina na sifa Zake. Ulimwengu huu unashuhudia kuwa na Muumbaji ambaye anastahiki kuabudiwa. Hakuna mwingine yeyote anayestahiki kuabudiwa. Ulimwengu mzima kukiwemo mbingu zake, ardhi zake, jua, mwezi, nyota, udongo, bahari na vyote vinavyopatikana vinamshuhudilia Allaah (´Azza wa Jall). Mshairi amesema:

Katika kila kitu kunayo alama

inayofahamisha kuwa Yeye ni Mmoja

Bi maana alama za kilimwengu. Kuhusu alama za Qur-aan ziko wazi juu ya suala hili. Zote zinajulisha uwepo wa Allaah na zinaamrisha kumtambua, kumwabudu, kujikurubisha Kwake na kutafuta radhi Zake.

[1] 7:59

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 65
  • Imechapishwa: 04/08/2024