Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Ni jambo la muhali ikawa zile karne bora – karne ambayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametumwa ndani yake, kisha wale wenye kuwafuatia kisha wale wenye kuwafuatia – walikuwa hawajui na hawaamini haki ya wazi juu ya mada hii.

MAELEZO

Ni jambo lisilowezekana kabisa zile karne zilizokuja baada ya Maswahabah na wakajifunza elimu kutoka kwao eti walighafilika na mada hii na wakaamua kutoifikisha. Tunawakusudia wanafunzi wa Maswahabah na wanafunzi wa wanafunzi wa Maswahabah, ambao wamesifiwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale aliposema:

”Wabora wenu ni karne yangu, kisha wale watakaofuata, kisha wale watakaofuata.”[1]

Karne bora ni tatu, au nne kwa mujibu wa baadhi ya mapokezi. Haiwezekani kabisa ikawa vizazi hivi bora hazikufikisha jambo hili kutoka kwa Maswahabah na badala yake wakaliacha hivi tu. Haiwezekani eti walikuwa tu wanasoma Qur-aan na Sunnah pasi na kufahamu maana yake. Hivo ndivo wanavyowatuhumu Jahmiyyah na vifaranga vyao. Wanaona kuwa karne hizi walikuwa wanafikisha maandiko pasi na kujua maana yake. Hii ni tuhuma mbaya mno kwa kizazi cha watu bora kabisa.

[1] al-Bukhaariy (2651) na Muslim (2535).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 67
  • Imechapishwa: 04/08/2024