35. Mfungaji anayetokwa na damu puani na damu ya ugonjwa

Himdi zote njema anastahiki Allaah. Swalah na amani zimwendee Mtume wa Allaah, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

Ama baada ya hayo;

1 – Damu yenye kutoka puani, yenye kutoka kwenye majeraha na damu ya maupele au majipu. Hizi haziathiri funga. Bali swawm ni sahihi.

2 – Damu ya ugonjwa inayomtoka mwanamke pia haiathiri funga. Bali swawm yake ni sahihi pamoja na kuendelea kwake kutoka kama ambavo haimzuii kuswali, kutufu Ka´bah na kujamiiana na mumewe. Kwa sababu damu hii haina kidhibiti. Ni damu yenye kuendelea kama kutokwa na damu puani na kwenye majeraha. Wala hakuna dalili inayofahamisha kumzuia kutokamana na ´ibaadah hizi kama ambavo dalili za wazi zimefahamisha kumzuia kutokamana na ´ibaadah hizi kwa sababu ya kuwa na hedhi na damu ya uzazi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus fiy Ramadhwaan, uk. 53
  • Imechapishwa: 25/04/2023