Miongoni mwa ´Aqiydah ya watu wa haki ni kwamba wako baadhi ya waislamu waliokuwa wakimwabudu Allaah pekee waliotenda madhambi makubwa watakaoingia Motoni. Waislamu watakaa humo kwa kiasi cha madhambi yao kisha baadaye watatolewa nje kwa uombezi wa waombezi na kwa rehema za Mwingi wa huruma. Hivo ndivo zimepokelewa Hadiyth tele kutoka kwa mkweli na mwenye kusadikishwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Watatoka Motoni baada ya kuchomwa Motoni. Watamiminiwa maji ya Uhai ambapo wachipuke kama inavyochipuka mbegu iliyobebwa na mafuriko.”[1] Mpaka watakaposafishwa na kutengenezwa ndipo wataidhinishwa kuingia Peponi.”[2]

Baada ya wale waislamu waliokuwa wakimwabudu Allaah pekee kutolewa Motoni, basi mlango utafungwa juu ya wale makafiri. Kwa msemo mwingine hawatotoka nje milele. Amesema (Ta´ala):

عَلَيْهِمْ نَارٌ مُّؤْصَدَةٌ

”Juu yao ni Moto uliofungiwa kila kona.”[3]

Kitu kingine kinachoungana na msingi huu ni kuamini yale yanayopitika ndani ya kaburi ambapo roho hurejeshwa katika viwiliwili anapolazwa ndani ya kaburi lake, kuhojiwa na Munkar na Nakiyr kuhusu Mola, dini na Mtume Wake, maiti kufunguliwa mlango wa Peponi au mlango wa Motoni anapokuwa ndani ya kaburi lake na kwamba kaburi ima ni bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi au ni shimo miongoni mwa mashimo ya Motoni.

[1] Muslim (182).

[2] al-Bukhaariy (2440).

[3] 90:20

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Iymaan – Haqiyqatuhu wa Nawaaqidhwuh, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 25/04/2023