35. Majaribio ya Shaytwaan kumshawishi yule mgonjwa na nduguze

Maiti anaweza kujipenyeza kwa yule mgonjwa na kumfanya afikiri kuwa atawaacha jamaa na wapenzi wake na kuiacha dunia hii na kwenda sehemu ya upweke chini ya udongo ambapo yule maiti ahisi kuumia. Hapa ndipo kuna khatari mtu yule akaanza kumchukia Mola wake na kuchukia kukutana Naye. Kuna khatari vilevile shaytwaan akamfanya kutamka kwa njia ya hasira na kuwa na kipingamizi kwa Allaah.

Baada ya hapo akajipenyeza kwa wale ndugu zake na kuwashawishi jinsi mtu yule alivyokuwa mzuri na kwamba alikuwa na nafasi ya juu ili awachochee wale watu kulia ambako ni haramu na kufanya mambo ambayo hayafai kufanywa. Vilevile anamchochea yule mgonjwa kuhuzunika na kutengana na dunia hii. Kwa ajili hiyo ndio maana inatakiwa kwa makundi yote mawili wajitibu kwa njia ya Kishari´ah. Tayari tumeshayataja katika mlango wa kwanza na ndio maana hakuna haja ya kuyakariri tena.

Hakuna muumini yeyote anayekufa kisha atamani tena kurudi katika dunia hii hata kama atapewa dunia nzima. Isipokuwa shahidi tu. Anapenda kurudi ili apigane na kuuawa kwa mara nyingine alipoona thawabu kubwa zinazopatikana katika kufa shahidi. Imaam Ahmad amepokea katika “al-Musnad” yake ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna nafsi yoyote ya muumini na muislamu inayochukuliwa na Allaah (´Azza wa Jall) kisha itake kurejea kwenu hata kama itapewa dunia nzima na vilivyomo ndani yake.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 58-59
  • Imechapishwa: 14/10/2016