34. Yanayopendeza kwa mfungaji: Kumkumbusha mfungaji anayekula kwa kusahau

2 – Anayemuona mwenye kula au kunywa mchana wa Ramadhaan hali ya kusahau ilihali amefunga ni lazima kwake kumkumbusha. Haijuzu kwake kumnyamazia kama wanavofikiria baadhi ya watu wajinga. Kwa sababu kufanya hivo ni katika kuamrisha mema na kukataza maovu. Jengine ni kwa sababu kula na kunywa mchana wa Ramadhaan ni maovu. Mwenye kusahau anapewa udhuru. Lakini ni lazima kumkumbusha. Kwani kufanya hivo ni katika kusaidizana katika wema na kumcha Allaah. Amesema (Ta´ala):

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ

“Saidiane katika wema na kumcha Allaah.”[1]

Swalah na amani zimwendee Mtume wa Allaah, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

[1] 05:02

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus fiy Ramadhwaan, uk. 52
  • Imechapishwa: 24/04/2023