Ibn Jariyr amesema: Ya´quub bin Ibraahiym ametuhadithia: Ibn ´Ulayyah ametuhadithia, kutoka kwa Mahdiy bin Maymuun, kutoka kwa al-Waliyd bin Muslim ambaye amesema:
”Twalq bin Habiyb alienda kwa Jundub bin ´Abdullaah na kumuuliza kuhusu Aayah ya Qur-aan. Jundub akamwambia: “Itakuwa ni dhambi kwako kama ni muislamu na usiondoke mbele yangu.” Au alisema: ”Usiketi nami.”[1]
Maalik amesimulia kutoka kwa Yahyaa bin Sa´iyd, ambaye ameeleza:
”Wakati Sa´iyd bin al-Musayya alikuwa anaulizwa kuhusu tafsiri ya Aayah ya Qur-aan, husema:
“Sisi hatusemi kitu juu ya Qur-aan.”[2]
al-Layth amesimulia kutoka kwa Yahyaa bin Sa´iyd, ambaye ameeleza:
”Alikuwa hazungumzii isipokuwa tu yale yanayotambulika katika Qur-aan.”[3]
Shu´bah amesimulia kutoka kwa ´Amr bin Murrah, ambaye ameeleza:
“Bwana mmoja alimuuliza Sa’iyd bin al-Musayyab kuhusu Aayah moja ya Qur-aan. Naye akajibu: ”Usiniulize kuhusu Qur’an. Muulize yule ambaye anadai kuwa anajua kila kitu juu yake.”[4]
Akimaanisha ´Ikrimah.
Ibn Shawdhab amesema: Yaziyd bin Abiy Yaziyd amenihadithia:
”Tulikuwa tunamuuliza Sa’iyd bin al-Musayyab kuhusu halali na haramu. Yeye ndiye alikuwa mjuzi zaidi wa watu. Tunapomuuliza kuhusu tafsiri ya Aayah ya Qur-aan, basi hunyamaza kana kwamba hatukusikia.”[5]
Ibn Jariyr amesema: Ahmad bin ´Abdah adh-Dhwabbiy ametuhadithia: Hammaad bin Zayd ametuhadithia: ´Ubaydullaah bin ´Umar ametuhadithia:
”Nimekutana na wanazuoni wa Madiynah. Walikuwa wakiheshimu mno kusema kuhusu tafsiri. Miongoni mwao ni Saalim bin ´Abdillaah, al-Qaasim bin Muhammad, Sa´iyd bin al-Musayyab na Naafiy´.”[6]
Abu ´Ubayd amesema: ´Abdullaah bin Swaalih ametuhadithia, kutoka kwa al-Layth, kutoka kwa Hishaam bin ´Urwah, ambaye amesema:
”Sikuwahi kumsikia baba yangu akifasiri Aayah yoyote kutoka ndani ya Kitabu cha Allaah.'”[7]
Ayyuub, Ibn ´Awn na Hishaam ad-Dastawaa-iy amesimulia kutoka kwa Muhammad bin Siyriyn, ambaye amesema:
“Nilimuuliza ‘Ubaydah as-Salmaaniy kuhusu Aayah moja ndani ya Qur-aan ambapo akasema: ”Wameondoka wale waliokuwa wakijua kuhusu yaliyoteremshwa ndani ya Qur-aan. Hivyo basi mche Allaah na lazimiana na usawa uwezavyo.”[8]
Abu ´Ubayd amesema: Mu´aadh ametuhadithia, kutoka kwa Ibn ´Awn, kutoka kwa ´Ubaydullaah bin Muslim bin Yasaar, kutoka kwa baba yake, ambaye amesema:
”Ukisimulia kutoka kwa Allaah, basi simama kwanza na utazame kilichosemwa kabla na baada yake.”[9]
Hishaam ametuhadithia, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Ibraahiym, ambaye amesema:
”Maswahiba zetu walikuwa wakijiepusha kutafsiri na wakilitukuza.”[10]
Shu´bah amesimulia kutoka kwa ´Abdullaah bin Abiys-Swafar, aliyeeleza kwamba ash-Sha´biy amesema:
”Naapa kwa Allaah! Hakuna Aayah moja ambayo sikuwahi kuuliza juu yake, lakini inahusiana na kusimulia kutoka kwa Allaah.”[11]
Abu ´Ubayd amesema: Hushaym ametuhadithia: ´Umar bin Abiy Zaa-idah ametuzindua, kutoka kwa ash-Sha´biy, kutoka kwa Masruuq, ambaye amesema:
”Jihadharini na tafsiri! Kwani inahusiana na kusimulia kutoka kwa Allaah.”[12]
[1] Jaamiy´-ul-Bayaan (1/63).
[2] Jaamiy´-ul-Bayaan (1/62).
[3] Jaamiy´-ul-Bayaan (1/62).
[4] Jaamiy´-ul-Bayaan (1/63).
[5] Jaamiy´-ul-Bayaan (1/63).
[6] Jaamiy´-ul-Bayaan (1/62).
[7] Fadhwaa-il-ul-Qur-aan, uk. 229.
[8] Jaamiy´-ul-Bayaan (1/62).
[9] Fadhwaa-il-ul-Qur-aan, uk. 229.
[10] Fadhwaa-il-ul-Qur-aan, uk. 229.
[11] Jaamiy´-ul-Bayaan (1/63).
[12] Fadhwaa-il-ul-Qur-aan, uk. 229.
- Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 106-107
- Imechapishwa: 14/04/2025

Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 106-107
Imechapishwa: 14/04/2025
https://firqatunnajia.com/34-msimamo-wa-salaf-juu-ya-kufasiri-qur-aan/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)