Baadhi ya Salaf wamesema:

“Pengine mtu akaketi kati ya watu na wale alioketi nao wakamuona kuwa ni mwenye kukosa usemi. Si mwenye kukosa usemi; huyo ni mwanachuoni muislamu.”

Yule mwenye kuwatambua Salaf ataona kuwa hawakuacha kusema, kubisha, kugombana na ufaswaha wenye kuzidi usiokuwa na haja kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kusema, ujinga wala upungufu. Walinyama kutokana na kujichunga na kumwogopa Allaah na kuacha kujishughulisha na yale mambo yasiyowanufaisha na badala yake kuyaendea yale yenye kuwanufaisha.

Walikuwa na msimamo huohuo katika mambo yote, ni mamoja misingi ya dini, mambo ya mataga, tafsiri ya Qur-aan na Sunnah, kuipa nyongo dunia, mambo ya kulainisha nyoyo, hekima, mawaidha na mengineyo waliyoyazungumzia. Yule mwenye kufata njia yao ameongoka. Na yule mwenye kufata njia isiyokuwa yao na akaingia katika kuulizauliza maswali mengi, kutafiti, kubisha na porojo, basi hali yake ni ya wastani ikiwa anatambua ubora wao na upungufu wa nafsi yake. Iyaas bin Mu´aawiyah amesema:

“Hakuna yeyote asiyetambua mapungufu ya nafsi yake isipokuwa atakuwa ni mpumbavu.” Ndipo akaambiwa: “Ni mapungufu yepi ulionayo?” Akasema: “Maneno mengi.”

Na ikiwa pamoja na hivo atajidai kuwa na ubora  na upungufu na ujinga kwa wale watangu wake, basi kwa hakika amepotea upotofu wa wazi na kukhasirika khasara kubwa.

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf, uk. 87-88
  • Imechapishwa: 30/09/2021