37. Du´aa anayeogopa dhuluma ya mtawala

  Download

129-

أللَّهُمَّ رَبَّ السَّمواتِ السَّبْعِ وَرَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيم، كُنْ لِي جاَراً مِنْ فُلانِ بْنِ فُلاَنٍ وَأَحْزَابِهِ مِنْ خَلاَئِقِكَ أَنْ يَفْرُطَ عَلَيَّ أحَدٌ مِنْهُمْ أَوْ يَطْغَى، عَزَّ جاَرُكَ وَجَلَّ ثَناَؤُكَ، وَ لاَ إِلَهَ إلاَّ أَنْتَ

”Ee Allaah! Mola wa mbingu saba, Mola wa ‘Arshi tukufu, kuwa mlinzi wangu kutokamana na fulani bin fulani na vikosi vyake katika viumbe Vyako, kwa kunisaliti mmoja miongoni  mwao au akanichupia mipaka. Imeimarika ipasavo hifadhi Yako na zimetukuka sifa Zako; hapana mungu wa kweli isipokuwa Wewe.”[1]

130-

الله أكْبَر، الله أعَزُّ مِنْ خَلْقِهِ جَمِيْعاً، الله أعَزُّ مِمَّا أخَافُ وَأحْذَر، أعُوذُ بِاللهِ الَّذِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ، الْمُمْسِكِ السَّمَوَا تِ السَّبْعِ أَنْ يَقَعْنَ عَلَى الأَرْضِ ِإلاَّ بِإِذْنِهِ، مِنْ شَرِّ عَبْدِكَ (فلان) وَجُنُوْدِهِ وَأَتْبَاعِهِ وَأَشْيَاعِهِ، مِنَ اْلجِنِّ والإِنْسِ، اَلَّلهُمَّ كُنْ لِيْ جَاراً مِنْ شَرِّهِمْ، جَلَّ ثَنَاؤُكَ وَعَزَّ جَارُكَ، وَتَبَارَكَ اسْمُكَ، وَلاَ إلَهَ غَيْرُكَ

“Allaah ni mkubwa, Allaah ni Mwenye nguvu na mshindi kuliko viumbe Wake wote. Allaah ni Mwenye nguvu na mshindi kuliko kile ninachokiogopa na kujihadhari. Najilinda kwa Allaah, ambaye hapana mungu wa kweli isipokuwa Yeye; Ambaye  amezizuia mbingu saba zisituangukie ardhi isipokuwa kwa idhini Yake, kutokamana na shari ya mja  Wako fulani na wanajeshi na wafuasi wake, miongoni mwa majini na watu.  Ee Allaah! Kuwa Mlinzi wangu kutokamana na shari yao. Zimetukuka sifa Zako, imeimarika ipasavo hifadhi Yako, limebarikika Jina Lako na hapana mungu wa haki asiyekuwa Wewe.”

Mara 3[2].

[1] al-Bukhaariy katika ”al-Adab-ul-Mufrad” (707). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh al-Adab-il-Mufrad” (546).

[2] al-Bukhaariy katika ”Adab-ul-Mufrad” (708). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh al-Adab-il-Mufrad” (546).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 29/04/2020