33. Uwajibu wa kusoma al-Faatihah katika kila Rak´ah

Alimwamrisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yule mwanaume mwenye kuswali kimakosa kusoma al-Faatihah katika kila Rak´ah. Alisema kumwambia baada ya kumuamrisha kusoma al-Faatihah katika ile Rak´ah ya kwanza[1]:

“Halafu ufanye hivo katika swalah yako yote.”[2]

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Halafu ufanye hivo katika kila Rak´ah.”[3]

Wakati mwingine alikuwa anaweza kuwasikilizisha Aayah[4].

Mara nyingine walikuwa wanaweza kusikia namna anavyoiremba “al-A´laa” na “al-Ghaashiyah”[5].

Wakati mwingine akisoma Suurah “al-Buruuj”, “at-Twaariq” na mfano wake[6].

Mara nyingine akisoma (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Suurah “al-Layl” na mfano wake[7].

[1] Abu Daawuud na Ahmad kwa mlolongo wa wapokezi ulio na nguvu.

[2] al-Bukhaariy na Muslim.

[3] al-Bukhaariy na Muslim.

[4] Ahmad kwa mlolongo wa wapokezi mzuri.

[5] Ibn Khuzaymah katika ”as-Swahiyh” (2/67/1) na adh-Dhwiyaa’ al-Maqdisiy katika ”al-Mukhtaarah” kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh.

[6] al-Bukhaariy katika ”Juz’-ul-Qiraa-ah” na at-Tirmidhiy aliyesema kuwa ni Swahiyh.

[7] Muslim na at-Twayaalisiy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 99-100
  • Imechapishwa: 06/02/2017