32. Kisomo cha Qur-aan katika zile Rak´ah mbili za mwisho

Alisoma (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Aayah katika zile Rak´ah mbili za mwisho baada ya al-Faatihah.

Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akizifanya Rak´ah mbili za mwisho fupi kuliko zile mbili za mwanzo, kiasi cha nusu yake na kiasi cha Aayah kumi na tano[1].

Wakati mwingine huenda akasoma ndani yake al-Faatihah peke yake[2].

[1] Ahmad na Muslim. Hadiyth hii inathibitisha kuwa ni Sunnah kusoma katika zile Rak´ah mbili za mwisho baada al-Faatihah Suurah. Haya ndio matendo ya Maswahabah akiwemo Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh). Maoni haya yamechaguliwa na Imaam ash-Shaafi´iy pasi na kujali sawa ikiwa swalah ni Dhuhr au nyengineyo. Miongoni mwa wanachuoni wetu waliokuja nyuma ambao wana maoni hayo ni Abul-Hasanaat al-Laknawiy katika “at-Ta´liyq al-Mumajjad ´alaa Muwattwa´ Muhammad”. Amesema:

“Baadhi ya wenzetu wana maoni ya ajabu pindi wanaposema kuwa ni wajibu kuleta Sujuud-us-Sahuw iwapo mtu atasoma kitu katika Rak´ah mbili za mwisho. Maoni haya yameraddiwa pamoja vilevile na Ibraahiym al-Halabiy na Ibn Amiyr Hajj kwa njia nzuri kabisa. Wale waliosema hivo bila shaka hawakufikiwa na Hadiyth, vinginevyo wasingelisema hivo.” (Uk. 102)

[2] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 99
  • Imechapishwa: 06/02/2017