33. Ni ipi hukumu ya kupangusa chini ya soksi za ngozi?

Swali 33: Ni ipi hukumu ya kupangusa chini ya soksi za ngozi?

Jibu: Kufuta chini ya soksi za ngozi sio Sunnah. Imepokelewa katika vitabu vya Sunan kwamba ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiay Allaahu ´anh) amesema:

”Laiti dini ingelikuwa inaenda kwa mapendekezo ya mtu basi kufuta kwa chini ya soksi za ngozi kulikuwa na haki zaidi kuliko kufuta kwa chini yake. Nilimwona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akifuta sehemu ya juu ya soksi zake za ngozi.”

Hili linafahamisha kwamba kilichowekwa katika Shari´ah ni kupangusa ile sehemu ya juu peke yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/177)
  • Imechapishwa: 06/05/2021